Na Hamida Kamchalla, Tanga.
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwasili mkoani Tanga siku ya kesho tarehe 20 kwa ziara ya siku tatu kwa lengo la kukagua ufufuaji wa zao la mkonge.
Akiongea na waandishi wa habari leo ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Martin Shigela amesema kuwa Waziri mkuu atawasili kesho saa tatu asubuhi na kuanza kutembelea kitalu cha chuo cha utafiti cha Mlingano na kugawa mbegu na kufuatilia utekelezaji wa fedha za mbegu shilingi milioni 700 alizozitoa.
Aidha Shigela ameeleza kwamba baada ya hapo Waziri Majaliwa atafanya mkutano na wadau wa kilimo cha mkonge katika ukumbi wa Legal Naivera na baadaye kuendelea na ziara yake hadi tarehe 22 atakapomaliza na kuondoka mkoani hapa.