Bi Harris mwenye umri wa miaka 55, aliondoka kwenye kinyang’anyiro cha kuwania urais mwezi Disemba baada ya kutofanikiwa kushinda katika mchuano wa uteuzi wa kiti cha urais wa chama cha Democratic.
Akikabiliana mara kwa mara na Bwana Biden wakati wa midahalo ya uchaguzi za awali , ambapo alikosoa jinsi Biden alivyosifu mahusiano ya ”kiraia” ya kikazi aliyokuwa nayo na seneta wa zamani ambaye alipendelea ubaguzi wa rangi.
Kamala alizaliwa katika Oakland, California, na wazazi wahamiaji :Mama yake alikua ni muhindi na baba yake Mjamaica.
Alisoma hadi Chuo Kikuu cha Howard , ambacho ni moja ya vyuo maarufu walivyosomea watu weusi kihistoria. Alielezea muda wake chuoni hapo kama moja ya maeneo yaliyojenga maisha yake.
Uchambuzi
Wakati mwingine uteuzi unaotarajiwa ni kwa ajili ya sababu inayotarajiwa.
Kamala Harris alikua wa mstari wa mbele katika wagombea wa Makamu wa rais hususan tangu wakati ulipotangazwa uteuzi wa Democratic mwezi Machi ambapo Biden alitangaza kuwa atamteua mwanamke kwa tiketi ya mgombea mwenza.
Ni mdogo kwa umri na mwenye nguvu za kuzungumza katika televisheni, na kama binti wa uhamiaji Mjamaica na Muhindi anawakilisha kuongezeka kwa utoaji wa fursa kwa watu wa jamii mbalimbali katika chama cha Democratic.
Zaidi ya hayo, anafahamika kupitia vyombo vya habari, kwa kampeni zake za kuwania urais mwaka 2019 na kwa muda katikakati ya mwaka jana baadhi ya kura za maoni zilimuweka katika nafasi ya kwanza.
Wengi miongoni mwa mahasimu wake katika kuwania kiti cha makamu wa rais hawakufikia kiwango cha kuchunguzwa cha aina hiyo, kwa hiyo hapakua na ushahidi kwamba wangeweza kuhimili wadhifa huo.
Faida nyingine aliyokuwa nayo ambayo inapuuzwa kumuhusu Bi Harris ni urafiki aliokuwa nao na Marehemu mtoto wa kiume wa Bwana Biden, ulioanzishwa wakati wote walipokua wanasheria wakuu.
Bwana Biden anathamini sana familia -na uhusiano huo huenda ulimrahisishia kumchagua.
Je anatosha kuongoza?
Baadhi ya wachambuzi wanasema wanawake wanapaswa kujithibitisha kwenye kampeni kwa njia ambazo wanaume hawafanyi, hata kama jinsia haiwatii hofu wapiga kura.
Pale ambapo watu wanachukulia uwezo kwa wanaume ni jambo la kawaida, wanawake lazima waonyeshe.
Kura ya maoni iliyofanywa na Economist/YouGov mwezi Agosti ulionyesha kuwa makamu wa rais aliyepo madarakani aliongoza kwa uchache wa kura za watu wanaompendelea akilinganishwa na bi. Harris.
Robo ya Wamarekani walioshiriki kura hiyo ya maoni hawakuwa na uhakika kuhusu uongozi wa Bi Harris, huku asilimia 14 wakitoa kauli sawa na hiyo kumhusu Bw. Pence.
Baada ya mjadala huo baadhi ya wapiga kura walihisi Harris alishinda.
Lakini walipoulizwa ni nani bora kuchukua nafasi ya rais baadhi yao walionekana kuwa na mtazamo tofauti.

Ni hali “ngumu kwa wanawake”, anasema, kwasababu ikiwa hawana watoto wala kuwazungumzia maswali yanaibuliwa “kwanini?” “Halafu wakiwazungumzia hasa wakiwa wadogo unaulizwa ni nani atawatunza watoto wako linaibuka?”
Hali ni tofauti kwa wanaume, wakati mwanamume anapozungumzia familia yake, anajenga taswira ya kuwa “kiongozi wa familia”, lakini “hakuna mtu yeyote anayemuuliza jinsi anavyowajibikia familia [yake]”, au hata kuuliza ni nani atawatunza watoto.
Mfano mzuri wa kufafanua hali hii ni kupitia Sarah Palin ambaye mjadala kuhusu familia yake ilizua gumzo alipoteuliwa kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi wa 2008.
Bi Palin ambaye alikuwa gavana wa jimbo la Alaska alijipata akielezewa darubini na vyombo vya habari na wafuasi wa Democratic waliotaka kubaini jinsi alivyo wajimbikia familia yake.
Wakati huo Bi Palin alikuwa na watoto watano na mmoja alikuwa na ulemavu. Wakosoaji wake waliuliza ikiwa atatelekeza familia yake kugombea nafasi ya juu ya uongozi.
Lakini hali hiyo ya ubaguzi wa kijinsia dhidi ya wanasiasa wa kike imeanza kubadilika – japo inakuwa vigumu kwa wanawake katika siasa kuepuka swali uzazi.
Bi Walshpia anaongeza kuwa Kamala Harris yuko katika nafasi ya kipekee kama mama kwa watoto wa kambo ambao sasa ni watu wazima.
Na ki uhalisia, wapiga kura wanataka kuwaona wagombea wao kama wanadamu wa kawaida waliyo na maisha yao binafsi.
“Kwa hivyo nadhani anafanya jambo ambalo la kiuhalisia”
Wanaume walisema nini kumhusu?
Donald Trump amemkumbuka vizuri sana, usiku wa Jumanne alisema, “Harris alikuwa mbaya kwa mtu wa pili alieteuliwa katika Mahakama ya juu zaidi aliymuonesha maudhi, Brett Kavanaugh.
Bw. Trump aliongeza kuwa ni mtu mwenye misimamo mikali na asiye na heshima n mwenye chuki: Hayo ndio maneno aliyotumia kumuelezea Harris alipokuwa mgombea mwenza wa Joe Biden.
Mpinzani wake Mike Pence hakutumia maneno ya matusi dhidi yake, lakini alimrushia madongo wakati wa mdahalo wa makamu wa rais .
Kamala Harris alipoanzisha kampeni yake mbele ya maelfu ya wafuasi wake Januari 2019, alichukuliwa kama mgombea wa juu. Wakati fulani, Julai, baada ya mdahalo wa kwanza aliokuwa amebobea, aliongeza ushawishi wake katika kura za maoni za awali.
Harris amepitia changamoto zake na anajua mtu anaweza kukumbana na yapi. Kama angekuwa mtu dhaifu, tayari angekuwa ameshafahamika kufikia sasa lakini almuradi ameamua kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kugombea kiti cha juu zaidi, inawezekana siku moja Wamarekani wakaanza kumfikiria kama rais.
Mambo yamebadilika vipi?
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Bi Walsh anasema mwaka 2018, ulishuhudia ongezeko kubwa la wanawake waliojitosa katika kinyang’anyiro cha kuwania nyadhifa za kisiasa’
“Wanawake hawakutumia muda mwingi kufukiria ‘natakiwa kufanya nini’ bali walijinadi wao kama wao,” anasema. “Tulishuhudia hilo mwaka 2018 wakati wagombea wengi walikuwa wakizungumzia masuala ambayo wanawake wameshauriwa kujitenga nayo.”
Masuala hayo ni kama kutotaja watoto wao, kuangazia changamoto yao maishania u kuzungumzia matatizo ya kifedha yanayowakabili.
Mwaka 2017, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice pia alitoa wito kwa wanawake kutokubali “mtu yeyote kuwabagua kwa misingi ya kijinsia au rangi ya ngizi yao”.
“Hiayo ni mambo lazima tuwaambie wanawake: Unapoingia katika chumba cha mkutano, ikiwa mtu atajaribu kukudunisha, usikabiliane naye. Unachotakiwa kufanya nikujieleza kwa utulivu bila hasira,” alisema lkatika kongamano la uongozi la KPMG.
“Ikiwa unahisi huenda umezuiliwa kitu ambacho unadhani ulistahili kupata, kuna njia nyingi ya kukitafuta – na una haki ya kihakikisha unakipigania hadi ukipate.”
Bi Walsh anasema kuanzia Geraldine Ferraro hadi kwa Sarah Palin na Hillary Clinton, kila mgombea amejiimarisha kutokana na tajiriba aliyopata zamani. Na sasa tumefikia kiwango ambacho mwanamke mweusi mwenye asili ya kihindi ameteuliwa kuwa mgombea mwenza wa urais “, alisema.
“Wakati wanawake wanapomuona mtu kama Kamala Harris akiteuliwa kama mgambea mwenza wa rais wanamchagua wakiwa na matumaini huenda akawa makamu wa rais, hatua hiyo tu inabadilisha mtazamo wa kile wanaweza kuwa maishani.”