Friday, January 10

RC Mattar “Madiwani wajibikeni”

 

MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoudi, amewataka madiwani wa mkoa huo kujiepusha na Rushwa Ubadhiri wa maali za umma na Ubaguzi wakati wanapowatumikia wananchi wanaowaongoza katika maeneo yao.

Alisema uwajipikaji wa viongozi kwenye nafsi zao, kunatoa mchango mkubwa wa kuimarisha amani na ummoja na kuchochea maendeleo kwa jamii.

Mkuu huyo wa Mkoa aliyaeleza hayo alipokuwa akifunguwa mdahalo wa kitaifa, kuhusu nafasi na mchango wa viongozi katika kulinda na kuimarisha amani, ummoja na kuchchea maendeleo ya wananchi wa Zanzibar, ulioandaliwa na Tasisi ya Mwalim Nyerere Foundation na kufanyika mjini Chake Chake.

Alisema migogoro migi duniani inasababishwa na matumizi mabaya ya madaraka, rushwa, ubadhilifu wa mali za umma hali inayopelekea kukosekana kwa amani, hivyo madiwani wanapaswa kusimamia hilo ili wananchi waendelee kuwa na imani na serikali yao.

“Suala la amani na utulivu ni jambo muhimu sana na linapaswa kuendelea kuhubiriwa, ili jamii iendelee kushikamana kuheshimiana katika kipindi chote hicho”alisema.

Mkuu huyo wa Mkoa alifahamisha kwamba zipo baadhi ya nchi za Afrika na Ulaya zimetumbukiwa katika vurugu, kutokana na matumizi mabaya ya rasilimali, hivyo madiwani wanawajibu wa kuliona hilo katika mabaraza yao, hususan katika matumizi mabaya ya fedha za serikali, pamoja na kusimamia kodi zinazokushwana na zitumike ipasavyo.

Akizungumzia suala la uwajibikaji, aliwataka madiwani na viongozi kuhakikisha wanawajibika ipaswavyo kwenye nafasi zao, pamoaja na kusimamia majukumu yao kikamilifu hususan katika suala zima la uwajibikaji.

Hata hivyo aliipongeza taasisi ya Mwalim Nyerere Foundation kwa kuwatumikia wananchi, kwani nia na madhumuni ni kubadilisha maisha ya wananchi, huku mikakati ya serikali kubadilisha mazingira ya kisiwa cha Pemba, kwa kuwekezwa viwanda mbali mbali na kutoa ajira kwa wananchi.

“Jamii ya Pemba kipo tafauti na maeneo mengine katika suala zima la siasa, vizuri kuendelea kuelimishana juu ya sauala zima la amani na utulivu katika kuwaleta watu pamoja”alisema.

Naye mkurugenzi Mtendaji na Mjumbe wa Bodi ya wadhamini wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation Joseph Butiku, aliwataka madiwani kuhakikisha wanashirikiana pamoja na kusimamia suala zima la amani na utulivu uliopo nchini, ikizingatiwa madiwani ndio wanaofika kwa wananchi vijijini.

“Baada ya uchaguzi kumalizika nchi zote duniani hali inakuwa tete, suala la amani hupotea na juhudi mbali mbali huchukuliwa ili kurudisha amani, madiwani nafasi yenu kuwaelimisha wananchi juu ya suala hilo”alisema.

Alisema panapokuwepo na amani na umoja hata maendeleo hayako mbali kufika, hivyo aliwataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kudumisha amani na umoja wao uliopo.

Hata hivyo aliwataka wananchi kutambua kuwa siasa ni maendeleo ya watu, kwani siasa isiyo na amani wala maendeleo hiyo imeshapitwa na wakati na haiendani na serikali ya awamu ya nane.

Mrajis wa NGOs Zanzibar Ahmed Khalid Abdulla, aliipongeza taasisi ya Malimu Nyerere Foundation kwani kazi yake kubwa kuhakikisha Tanzania inabaki salama na sehemu ya amani duniani.

Hata hivyo alimpongeza Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi, kuhakikisha amani inaendelea kudumu muda wote, pamoja na kuendelea kusimami maridhiano yaliyopelekea uwepo wa serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Kwa upande wake Hamad Abdalla Hamad diwani wa wadi ya Vitongoji kuchaguliwa, alisema atakahakikisha suala la amani na utulivu linaendelea kutolewa kwa wananchi wote hususana vijijini.

Naye Mayasa Said Mohamed Diwani wa wadi ya Kangani, alipongeza taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation kwa kuendelea kuwakumbusha juu ya suala zima la kuendelea kuhubiri amani na utulivu.