Thursday, January 9

Tatuweni kero za wananchi: RC Kaskazini Pemba.

NA ABDI SULEIMAN.

MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib, amesema madiwani wanapaswa kufuatilia kwa vitendo kero zinazo wakabili wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, bila ya ubaguzi wowote pamoja na kusimmia utekelezaji wa fedha za miradi ya maendeleo ndani ya wadi zao

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwamba madiwani wanawajibu mkubwa wa kusimamia fedha za walipa kodi, ili wananchi wawezekuona zinatekelezwa katika miradi ambayo inaleta tija kwa wanachi na kunufaika nayo, bila ya kutoa rushwa wala kuwepo kwa harufu ya ubadhirifu wa mali.

Alisema kufanya hivyo kutapelekea kujenga ummoja mashirikiano na kudumisha amani ya nchi iliyopo, kwani kutapelekea kuepukana na migogoro mingi inayotokea katika jamii.

Mkuu huyo aliyaeleza hayo alipokuwa akifungua mdahalo wa kitaifa, kuhusu nafasi na mchango wa viongozi katika kulinda kuimarisha amani na umoja, na kuchochea mendeleo ya wananchi wa  Zanzibar kwa madiwani wa mkoa wa kasikazini Pemba, mdahalo uliondaliwa na Tasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation huko mjini Wete.

Alisema taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation imeweka mdahalo huo, kwa lengo la kuwaonyesha njia madiwani katika kujenga Ummoja wao na kuwatumikia wananchi ipasavyo.

Akizungumzia suala la amani na utulivu, alisema iwapo madiwani wataondosha dhulma, Rusha na kuwajibika ipasavyo basi amani na utulivu itakuwepo ya kutosha, ndio maana Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation imeamua kutoa elimu hiyo.

“Waasisi wa taifa hili walikuwa wakipinga rushwa na kuhimiza umoja, mshikamano na maedeleo bora kwa wananchi, sisi ambao tumepewa na fasi za kuwaongoza wananchi tunawajibu wakuwa mstari wambele katika kupinga hayo”alisema.

“Sote tunakumbuka na tunasikia kauli za mwasisi wa chuo hichi Mawilimu Nyerere,  Mwalimu alipiga vita rushwa na kusema kama ni aduia wa haki, na sisi tunapaswa kutekeleza kwa vitendo kauli hiyoo”alisema.

Hata hivyo aliwataka madiwani hao kubuni vyanzo vipya vya mapato, ambavyo vitaweza kuongeza kipato kwa baraza au halimashauri na kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi wanao waongoza.

Mkurugenzi Mtendaji wa tasisi ya Mwalimu nyererr Foundation Joseph Butiku, alisema kupatikana kwa maendeleo sehemu yoyote kunahitajika kuwepo kwa amani, umoja na mashirikiano ya pamoja, ndio maana mwalimu alikuwa akihimiza hayo akiamini kuwa ndio msingi wa maendeleo kwa wananchi.

“Umoja na Mashirikiano ya pamoja yanaoneshwa na viongozi wa Zanzibar, kataika kunda serekali ya umoja wa kitaifa ni hatua mmoja mzuri, wakiwa na nia ya dhati ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar kwa kuondoa migogoro na mifarakanpo kwa jamii”alisema.

Akitoa mada Maendeleo ya Wananchi kama nguzo ya Amani na Umoja wa Kitaifa nchini Tanzania, Msaidizi Maalum wa Mkurugenzi Mtendaji wa Tasisi ya Mwalim Nyerere Foundation Mzee Gallus Abedi, alisema maendeleo kwa wanachi hutolewa kwa kuboresha huduma za kijamii, kwa kuanzia ngazi ya wadi madiwani ambapo wanawajibu wa kusimamia ndani ya maeno yao.

Alisema  maendeleo yananza ngazi ya chini katika wadi, kataa kwa viongozi kuhakikisha wanazitoa kero zote zinazo wakabili wananchi, kufanya hivyo kutapatikana maendeleo na kutaepusha migigoro inayotokeza kwani wananchi wanahitaji huduma bora kutoka kwa viongozi waliowachagua.

Mrajis wa jumuiya zisizo za serekali Zanzibar Ahmed Khalid Abdulla alisema, upatikanaji wa maendeleo yanaendana sambamba na udumishwaji wa amani, hivyo kila mmoja anawajibu wa kusimamia hilo kuanzia kwa viongozi wakuu, hata mtu mmoj mmoja kwani kwenye amani ndiko kunako patikana utawala bora na huduma mzuri kwa wanachi.

Nao Madiwani hao wameishukuru tasisi ya Mwalim Nyeyere kwa mdahalo huo, kwani umekuja wakati muafaka na umewajengea uwezo mkubwa wa kuweza kutumikia vizuri.