Friday, November 15

Virusi vya Corona: Uingereza yapiga marufuku abiria kutoka Tanzania,DRC

Uingereza yapiga marufuku abiria kutoka Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuzuia maambukizi ya aina mpya ya virusi vya corona.

“Abiria wote kutoka Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo hawataruhusiwa kuingia nchini Uingereza na katika mataifa ya Irish kuanzia saa kumi alfajiri,” amesema Grant Shapps, waziri wa usafirishaji nchini Uingereza.

Kuanzia tarehe 22 Januari, saa kumi alfajiri wasafiri wote kutoka au wamepita nchini Tanzania ndani ya siku 10 hawataruhusiwi kuingia Uingereza na mataifa ya Irish, na wale ambao wana haki ya makazi nchini Uingereza na wanatoka Tanzania watahitaji kujitenga nyumbani kwao watakapowasili.

Katika masharti mapya nchini Uingereza dhidi ya Corona, lazima watu wabaki nyumbani au kutosafiri, pamoja na kutosafiri nje ya nchi labda tu ukiwa umeruhusiwa kwa kibali maalum kufanya hivyo.

Tanzana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimeongezwa kwenye orodha ya Uingereza ya nchi zilizopigiwa marufuku ya wasafiri wake kuingia nchini humo kama hatua yza kudhibiti maambukizo ya aina mpya ya virusi vya Corona vilivyogunduliwa nchini Afrika kusini.

Marufuku hiyo itaanza rasmi Jumamosi na itakuepo kwa muda wa wiki mbili , serikali ya Uingereza imesema.

“Uingereza ilipiga marufuku wasafiri kutoka mataifa 11 ya Afrika Kusini siku 10 zilizopita , mataifa hayo ni pamoja na Namibia, Zimbabwe, Botswana, Eswatini, Zambia, Malawi, Lesotho, Msumbiji na Angola – visiwa vya ushelisheli na Mauritius,” taarifa kutoka idara ya usafirishaji imesema.

Aliongeza kusema kuwa “Israel itaondolewa katika orodha ya mataifa yaliyopigwa marufuku kuingia Uingereza na watu waliowasili Januari 09 kutoka Botswana, Israel , Mauritius au visiwa vya shelisheli watahitajika kujitenga wenyewe kwa muda.”

Awali Uingereza ilipiga marufuku abiria kutoka Afrika Kusini Desemba 24,na kuruhusu wale walio na visa pamoja na haki ya makazi nchini Uingereza na watakapowasili watahitajika kujitenga kwa muda wa siku 10.

Uingereza ni miongoni mwa mataifa ambayo yanakabiliana na janga la virusi vya corona kwa kiwango kikubwa na uchumi wake ukiwa umeyumba kutokana na wimbi la kwanza la virusi mambukizi ya corona.

Wakati mataifa mengine yakipambana na janga hili Rais wa Tanzania John Magufuli alisema mwezi Juni mwaka jana kuwa taifa lake ‘lipo huru na maambukizi ya virusi vya corona’ shukrani kwa maombi.

Hata hivyo Shirika la Afya duniani (WHO) lilieleza wasiwasi wake juu ya hatua zinazochukuliwa na taifa hilo dhidi ya kukabiliana na Covid-19.

Serikali ya Tanzania imeondoa marufuku ya wageni wanaoingia nchini humo kukaa karantini kwa muda wa siku 14-,pamoja na kutaka wageni kuonesha vyeti vya vipimo vya COVID-19 vinavyowaonesha kuwa hawana maambukizi.

Ingawa huwa wageni huwa wanapimwa joto wanapowasili.Kama wataonekana na dalili COVID-19 ndio watahitajika kujitenga kwa muda wa siku 14.

Kufuatia hatua hiyo ya Uingereza kutangaza marufuku dhidi ya wasafiri wa Tanzania, si mamlaka ya Tanzania au DRC yamezungumzia juu ya suala hilo.

 

ADVERTISEMENT