Nusu ya uwekezaji mpya nchini Marekani kutoka katika makampuni ya kigeni ulishuka mwaka uliopita hatua iliosababisha taifa hilo kupoteza nafasi yake ya kwanza.
Kwa upande mwingine, takwimu hizo zinaonyesha uwekezaji wa moja kwa moja katika kampuni za Wachina uliongezeka kwa asilimia 4 , na kulifanya taifa hilo kuchukua nafasi ya kwanza duniani.
Kupanda kwa China kunaonesha ushawishi wake katika sekta ya kiuchumi duniani.
China ilijipatia kipato cha $163bn (£119bn) mwaka uliopita , ikilinganishwa na $134bn zilizoingia Marekani, Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na Maenedeleo (UNCTAD) ulisema katika ripoti yake.
Mwaka 2019, Marekani ilipokea $251bn kupitia uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni huku China ikijipatia$140bn.
Huku China ikiwa katika nafasi ya kwanza kwa uwekezaji mpya wa kigeni, Marekani bado inatawala katika uwekezaji wa jumla kutoka mataifa ya kigeni.
Hii inaonyesha miongo ambayo imetumia kama eneo la kuvutia zaidi kwa wafanyabiashara wa kigeni wanaotafuta kupanua biashara zao ng’ambo.
Lakini wataalam wanasema takwimu hizo zinasisitiza hatua ya Uchina kuelekea katikati mwa uchumi wa ulimwengu ambao kwa muda mrefu umetawaliwa na Marekani, taifa lenye uchumi mkubwa zaidi duniani .
China , kwa sasa inayohusika katika vita vya kibiashara na Marekani , ilitabiriwa kwamba italipiku taifa hilo kufikia 2028, kulingana na kituo cha Utafiti wa kiuchumi na Biashara CBR kutoka Uingereza.
Kuanguka kwa Trump
Uwekezaji wa kigeni nchini Marekani ulipanda 2016 na kufikia $472bn, wakati uwekezaji wa kigeni China ulikuwa $134 bn.
Tangu wakati huo , uwekezaji nchini China uliendelea kupanda , huku Marekani ukishuka kila mwaka tangu 2017.
Pia ilionya kampuni na wawekezaji wa China kwamba watakabiliwa na uchunguzi mpya wakati wanapowekeza Marekani kwa kuzingatia misingi ya usalama wa kitaifa.
Huku Uchumi wa Marekani ukijinasua tangu mlipuko wa virusi vya corona mwaka uliopita, uchumi wa China umeshika kasi.
Ukuaji wa uchumi wa China, uliopimwa katika pato la taifa (GDP), ulikua kwa asilimi 2.3 mwaka 2020, kulingana na data rasmi mwezi huu.
Hii inaifanya China kuwa taifa la pekee duniani lililoepuka kushuka kiuchumi mwaka uliopita.
Wanauchumi wengi wameshangazwa na kasi ya kupona kwake , hususan wakati ambapo ilikuwa inapitia wakati mgumu katika uhusiano wake na Marekani.
Kwa jumla , uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja ulishuka mwaka 2020, ukipungua kwa asilimia 42 , kulingana na ripoti ya UNCTAD.
FDI kawaida uhusisha kampuni moja inayochukua udhibiti wa ile ilio ng’ambo kupitia ushirikiano ama ununuzi.
Uwezekezaji wa moja kwa moja wa kigeni ulishuka kwa asilimia 100 nchini Uingereza mwaka uliopita kutoka $45bn mwaka 2019 chini kutoka -$1.3bn.
|
|
|
|