IMEELEZWA kuwa jumla ya matundu 41 ya vyoo yanahitajika katika skuli ya Msingi na Sekondari Kojani Wilaya ya Wete, ikiwa na wastani wa wanafunzi 40 wanahitajika kutumia tundu moja la choo, kwenye wanafunzi 2083 wa skuli hiyoo.
Hayo yamebainika wakati wa hafla ya kukabidhi mifuko 20 ya saruji, iliyotolewa na mbunge wa jimbo la Kojani Hamad Hassan Chande, kwa uongozi wa kamati ya skuli hiyo kwa ajili ya ukarabati wa vyaoo vilivyopo skulini hapo.
Kwa sasa skuli hiyo inamatundu 16 ya vyoo na matundu manne tu ndio yanayofanya kazi kukiwa na upungufu wa matundu 25 ya vyoo kwa sasa.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi baadhi ya wanafunzi wanaosoma skuni hapo, wamesema kwa sasa hulazimika kwenda kujisaidia baharini au kwenye mikandaa.
Mwanafunzi Hakim Shaame Ali “sisi wanafunzi wa kojani tunakwenda kujisaidia Pwani, kwa sababu vyoo vyao ni vibovu na vinahitaji matengenezo”alisema.
Alisema kwa sasa imekuwa ni ngumu kupata sehemu salama ya kujisaidia, iwa vyoo vilivyopo skuli vitashindwa kufanya kazi hali itakayopelekea kuharibu mazingira.
Naye mwanafunzi Sada Omar Kai, alisema kuharibika kwa vyoo ni tatizo kubwa kwao, zaidi wanafunzi wa kike ikizingatiwa wengi wao ni wanafunzi wadogo.
“Kwa sasa tunae Pwani au vichakani, sisi wakubwa tunaenda kuomba majumbani, wakati mwengine hata vipindi tukifika vishamalizika”alisema.
Aidha alisema kama kungekuwa na vyoo vizima wasingepata tabua ya kwenda huko, wangetumia vyoo vya hapo hapo skuli huku akiwaomba wadau na wafadhili kujitokeza kusaidia ujenzi wa ukarabati na ujenzi wa vyoo vipya skulini hapo.
Mmoja ya walimu wa skulini hapo Mussa Ali Omar, alisema kukosekanji wa vyoo ni tatizo sugu skulini hapo, hasa wanafunzi wa kike wanapohitaji kujisaidia hulazimika kukimbilia majumbani.
Alisema wanapokwenda huko hutumia muda zaidi ya dakika 15 hadi 20, hali inayopelekea wakati mwengine kukosa baadhi ya masomo au topiki zinazofundishwa.
“Watoto wakike kwenda kujisaidia katika mikandaa (mikoko)au chochoroni ni jambo la aibu, walimu wanakimbilia misikitini kwa wanaume na wanawake majumbani”alisema.
Aidha nae mwalimu Mkuu wa Skuli ya Kojani Msingi na Maandalizi Khamis Ali Makame, alimpongeza mbunge wa jimbo la Kojani kwa kuunga mkono juhudi za skuli, katika ukarabati wa vyoo skuli hapo.
Alisema kufanyika kwa ukarabati huo wa vyoo utaweza kuwaondoshea usumbufu walimu na wanafunzi, katika sula zima la sehemu sahihi ya kujisaidia.
Aidha alipongeza jitihada kubwa zilizochukulia na baraza la mji Wete na Serikali kuu, lakini bado miundombinu ya vyoo haijawa mizuri kutumika.
“Pasipokua na vyoo vya kutosha afya za wanafunzi zitaathirika ikizingatiwa hichi ni kisiwa hakuna sehemu nyengine yoyote ya kujisaidia na idadi ya wanafunzi ni kubwa, aliwataka wadau kutoa mchango kwa maendeleo ya skuli na elimu zaidi,
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kojani Hamada Khatib Salim, alisema lengo la kukabidhi mifuko hiyo ya saruji ni utekelezaji wa ahadi alizozitoa mbunge wa jimbo hilo, katika kusaidia maendeleo ya skuli hiyo.
Aidha aliutaka uongozi wa kamati ya skuli, kuhakikisbha msaada huo wanautumia kwa malengo ya yaliyokusidiwa ili kuwaondoshea usumbufu wa toto wakike.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya skuli hiyoo Omar Abdalla Saidi, aliahidi kuwa ndani ya wiki moja kazi hiyo watakua wameshaifanya na huduma kurejea.
Skuli ya msingi na maandalizi Kojani ina wanafunzi 2083 wanawake 1104 na wanaume 999, huku wanafunzi 40 wanahitajika kutumia tundu moja la vyoo, skuli ikihitaji jumla ya matundu 41