Monday, November 25

Makongoro Nyerere”Wana CCM Pemba hongereni”.

MJUMBE wa Kamati kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa Mikoa Miwili ya Pemba Makongoro Julius Nyerere, amewashukuru wananchi na wanaCCM wa mikoa hiyo kwa kufanikisha Uchaguzi kwa amani na CCM kuongoza katika majimbo mengi ndani ya kisiwa hicho.

Alisema baada ya kuteuliwa na chama chake kuwa mlezi wamikoa hiyo, alianza kupata na hofu kutokana na kisiwa hicho kuwa ngome ya upinzani lakini viongozi waliopo wa Pemba wakamuahidi mambo makubwa, kwenye ngome ya upinzani imeweza kuvunjika.

Malezi huyo wa Mikoa ya Pemba aliyaeleza hayo mara baada ya kuweka jiwe la Msingi Tawi la CCM Mkoroshoni jimbo la Wawi Wilaya ya Chake Chake na kukabidhi mifuko 30 ya saruji iliyotolewa na mwakilishi wa jimbo hilo.

Alisema ushindi huo uliopatikana kwa CCM ni kukijengea heshima chama, pamoja nay eye kuonekana uwezo wake umeweza kusaidia na kujenga safu imara.

“Siku niliyopewa nafasi hii kwanza nilipatwa na hofu kubwa, ila sikuweza kuikataa nikasema mara hii katika mikoa yote ya Tanzania Pemba lazima uwe Mkoa wa kwanza kufanya vizuri katika Uchaguzi, vipo vigezo vingi na hilo litawezekana tusubiri majibu sasa”alisema.

Akizungumzia suala la Matawi ya kisasa ya Chama, alisema chama kimeagiza CCM lazima iwe na matawi mazuri ya wanachama wake pale wanapotaka kuzungumza mambo yao wawe katika sehemu salama na sio kukaa chini ya miti.

Alisema kukamilika kwa tawi hilo litaweza kujenga haiba nzuri kwenye chama na jimbo lake, huku akiwataka kukahikisha viongozi waliopo wanasimamia ipasavyo kukamilika kwa tawi hilo ndani ya mwezi mmoja na wanaCCM waweze kutumia.

“Haya ndio matawi tunayoyataka kwa sasa sio yale matawi ya kukaa pembeni na kuzungumza mambo yetu, kilichobaki ni kija tena nikute mambo yamebadilika hapa”alisema.

Kwa upande wake katibu wa kamati maalumu idara ya siasa na uhusiano wa Kimataifa Mwalim Kombo Hassan Juma, alisema haipendezi kuona vikao vinafanyika katika miti bali vinapaswa kufanywa katika matawi ya kisasa, kama ilivyo tawi la CCM Mkoroshoni.

Mjumbe wa kamati ya siasa ya Mkoa wa Kusini Pemba, pia ni Mkuu wa Mkoa huo Mattar Zahor Massoud, alisema upande wa serikali umejitahidi sana kuhakikisha chama kinarudi tena madarakani katika uchaguzi mkuu uliopita.

Kwa upande wake mwakilishi wajimbo la Wawi Bakar Hamad Bakar, alisema baada ya kuapishwa tu aliweza kazi ya utekelezaji jimboni kwenye maeneo mbali mbali, huku akiahidi kukabidhi mifuko 30 ya safuji na fedha za fundi kwa kupiga palasta.

Katika uwekaji wa jiwe hilo la msingi, Mjumbe huyo aliweza kupiga harambee na Jumla ya shilingi Milioni 1,595,000/= zilipatikana, keshi ni shilingi laki 835,000/= na ahadi ni shilingi 760,000/=, pamoja na mafeni manne na mifuko 10 ya saruji.