NA ABDI SULEIMAN.
ASASI za Kiraia nchini Tanzania zimeshauriwa kutumia mitandao ya kijamii, katika kuelezea umma mambo mbali mbali yanayofanywa na asasi hizo kwa jamii.
Ushauri huo umetolewa na mratib wa Program kutoka shirika la Internews Tanzania Shaban Maganga, wakati alipokua akifungua mafunzo ya siku tatu kwa njia ya mtandao wa ZOOM, kupitia Mradi wa kuboresha mahusiano baina ya vyombo vya habari na asasi za kiraia.
Alisema hivi sasa dunia imebadilika imekwua na watumizi wengi wa mitandao ya kijamii, hivyo ni vizuri munapokuwa na vikao kuwatumia waandishi wa habari kwa ajili kuwawekea katika mitandao hiyo.
Alifahamisha kuwa mitandao ya kijamii, hivi sasa imekuwa ikitumika katika kukuza na kutangaza uchumi wanchi, hivyo asasi hizo zinanafasi kubwa katika kutangaza mambo yao.
“Shirika la Internews limekuwa kifuambele, katika kutoa elimu na kufundisha baadhi ya waandishi na viongozi wa CSO juu ya kutumia mitandao kwa kuweka taarifa zao mbali mbali”alisema.
Naye afisa mradi kutoka Internews Tanzania Victoria Rowan, alisema mitandao ya kijamii imekuwa na nguvu sana kuleta maendeleo hivi sasa duniani.
Alifahamisha kuwa kupitia mitandao hiyo watu wamekuwa wakipata taarifa za waandishi na ndio hao hao wanaotumia mitandano hiyo ya kijamii.
Kwa upande wake Mkufunzi wa masuala ya Mitandao kutoka shirika hilo, Amini Suwedi alisema kuwa mitandao ya kijamii imekuwa ndio maisha ya kila siku kwa taasisi katika kuitaarifu jamii.
Aidha aliwataka washiriki wa mafunzo hayo, kuhakikisha wananchi waliowazunguka wanatumia mitandano ya kijamii vizuri, pamoja na kuangalia wananchi wanafuatilia taarifa zao kwa usahihi.
“Lazima tuwe na mahusiano na msomaji wetu, tunapaswa tuwe tunaweka kazi zetu na kufuatilia jee, kazi hizo zinapendwa na wasomaji na maoni ya wasomaji yanasema vipi”alisema.
Naye Leah Mushi kutoka Internews alisema bora kuwe na watu kidogo katika mtandao ili wapate kusoma kazi zako na kuliko kuwa na wingu la watu hakuna anaepitia, hapo utakuwa hujafanya kazi ya kushawishi watumiaji wako wa mitandao.
Katika hatua nyengine Wenceslaus Mushi kutoka Intenews, alisema CSO zinapaswa kujua jamii inahitaji kujua kazi zote na kipi zinazofanywa na CSO.
Alisema kazi kubwa ni kutengeneza njia kuu kushikamana na waandishi wa habari, pale wanapokuwa na vikao vyao kuhakikisha wanawaalika ili kuwatangazia taarifa zao.
Kwa upande wao viongozi wa Asasi za Kiraia, waliahidi kutumia mitandao ya kijamii katika kutangaza taarifa zao, pamoja na kuihabarisha jamii kujua CSO kazi zake.