Monday, November 25

Hakimu Lusiano Makoe Nyengo atoa mda kwa shahidi dokta kufika mahakamani kutoa ushahidi.

Kushindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi  juu ya kesi ya udhalilishaji kwa shahidi ambae ni daktari kumemfanya wakili msomi Ali Hamad Mbarouk kuiomba mahakama ya mkoa  Chake chake kuliondosha shauri hilo .

Akizungumza mbele ya hakimu wa mahakama hiyo lusiano Makoe Nyengo amesema tarehe iliyopita wakili mwenzangu alisema kwa vile shauri lishakua la muda mrefu litolewe uwamuzi, kwa hiyo leo tunaomba mahakama yako ifute  kesi hiyo.

‘’Mheshimiwa shauri hili lipo kwa muda mrefu sasa tunaomba ulifute shauri hili’’ alisema wakili msomi.

Wakili wa Serikali kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka [ DPP] Juma Ali Juma amekataa ombi hilo na kuitaka mahakama itoe tena muda kwani maelezo kutoka Polisi yanasema kuwa Dokta Abudu atakuwa hayupo mahakamani yupo safarini.

‘’Mheshimiwa hakimu maelezo yanasema dokta Aboud atakua  yupo safarini hivyo tunaomba utupe tena muda’’ alisema wakili wa serikali.

Hakimu wa mahakama ya mkoa Chake chake Lusiano Makoe Nyengo amekubaliana na ombi la wakili wa Serikali hivyo natoa tena muda hadi 22/April mwaka huu.

Kesi hiyo ya kutorosha na kulawiti mtoto wa kiume wa 10 inayo mkabili Hji Abrahman Mussa mwenye umri wa 20 mkaazi wa Kirimdomo kendwa Kiwani Pemba.

Imedaiwa mahakamani hapo mtuhumiwa huyo  siku ya 10/3/ 2020 majira ya sa sita mchana alitenda makosa mawili tofauti, kosa la kwanza alimtorosha mtoto wa kiume wa 10 wakati alipokua  njiani akirudi Skuli na kwenda nae  kwa utao jambo ambalo ni kosa kinyume na kifungu cha 113[1] [b] cha sheria ya adhabu nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.

Na kosa la pili  siku hiyo hiyo muda huo huo ulimlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 10  ambapo kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 115[1] cha sheria  ya adhabu sheria namba 6  ya mwaka 2018 sheria ya Serikali ya Zanzibar.