Monday, November 25

Kesi yaondolewa mahakamani kwa kutofika mashahidi.

Baada ya mashahidi wa upande wa anaedaiwa kufanyiwa udhalilishaji kushindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi kumemlazimu hakimu wa mahakama ya Mkoa Chake chake Lusiano Makoe Nyengo kuiondosha kesi ya kutorosha na kubaka inayomkabili mtuhumiwa Mohd Salim Rashid   mwenye umri wa 25 mkaazi wa Machomane Chake chake Pemba.

Baada ya mtuhumiwa kupanda kizimbani na kusikiliza maelezo kutoka mahakamani hapo mwendesha mashtaka kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka DPP Juma Ali Juma aliambia mahakama hiyo kuwa tarehe iliyopita ilikua aje kusikilizwa shahidi ambae ni daktari lakini hakufika mahakamani na akapewa onyo, na terehe ya leo hadi tunaingia mahakamani hayupo, hivyo tunaomba ighairishwe ipangwe siku nyengine.

‘’Mheshimiwa hakimu mimi naomba tuipange siku nyengine kwa ajili kumuita tena daktari’’, Alieleza DPP.

Wakili msomi alisema mimi napinga sikubaliani na  hayo na nakumbuka kwamba leo ni siku ya kutolewa mamuzi.

Hakimu wa mahakama ya mkoa Chake Lusiano Makoe Nyengo amesema nakubaliana na ombi lako kwa vile kesi ipo kwa muda mrefu mashahidi hawafiki mahakamani kutoa ushahidi, mahakama yangu imeamua kuliondosha shauri hilo.

Imedaiwa kuwa mtuhumiwa huyo aletenda makosa mawili tofauti, kosa la kwanza siku ya 3/12/ 2018  huko machomane Chake wilaya ya chake bila ya halali na bila ya ridhaa ya wazazi wake ulimtorosha msichana wa miaka 16 kutoka nyumbani kwao Wingwi na kwenda nae kwenye nyumba  unakoishi jambo ambalo ni kosa kinyume na kifungu cha 113[1] [a] sheria namba 6/2018 sheria ya Zanzibar.

Kosa la pili siku hiyo hiyo majira ya sa saba kamili za mchana ulimbaka msichana huyo wa miaka 16 kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 108[1] [2] [e] na 109 [1] sheria ya adhabu sheria nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.