Monday, November 25

“Suala la muhali katika serikali ya awamu ya nane halina nafasi” RC Kusini Pemba.

MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Masoud, akifungua mkutano wa wadau wa Operesheni na udhibiti wa dawa za kulevya Pemba, ulioandaliwa na Tume ya Kitaifa ya kuratibu na udhibiti wa dawa za kulevya, kutoka Ofisi ya Mkamu wa Kwanza wa Rais na kufanyika mjini Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 

MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Masoud, amewataka wadau wa Operesheni ya Udhibiti wa dawa za kulevya Kisiwani Pemba, kutambua kuwa suala la muhali katika serikali ya awamu ya nane halina nafasi, hivyo wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa kufuata taratibu na sheria.

Alisema ifike wakati wananchi wafahamu kuwa wasimamizi hao, wanadhamira ya kutekeleza matakwa hayo ya kutokomeza madawa ya kulevya katika jamii.

Mkuu huyo aliyaeleza hayo wakati alipokua akifungua mkutano wa wadau wa Operesheni na Udhibiti wa dawa za kulevya Pemba, mkutano uliofanyika mjini Chake Chake.

Aidha alifahamisha kuwa kila taasisi inawajibu wa kutekeleza majukumu yake katika suala zima la kutokomeza dawa za kulevya, hivyo mashirikianao na nia ya pamoja kwani hivyo ni vita vikubwa baina ya matajiri na serikali.

“Mapambano ya dawa za kulevya ni mapambano makubwa sana, wahusika hawatakuwa tayari kuona wanakatisha biashara zao na wanajipanga na sisi wasimamizi tukiwa kitu kimoja tutaweza kutokomeza hilo”alisema.

Hata hivyo aliwataka kuweka mbele uzalendo kwa ajili ya nchi na kuwanusuru vijana ambao ndio waathirika wakubwa wa madawa hayo, hukju akiwataka watumishi hao kutambua kuwa katika mkoa huo mtumishi atakaebainika kurudisha nyuma juhudi hizo basi hatokuwa na nafasi.

Kwa upande mwengine Mkuu huyo wa Mkoa, alisema tayari alishatoa maagizo maeneo yote ya nje ya vileo hayaruhusiwi kufanya biashara ya vileo, isipokua maneo ya vikosi vya ulinzi na usalama ambayo yako kisheria.

Naye afisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Ahmed Abubakar Mohamed, alisema mashirikiano ni kitu muhimu sana kwa wadau hao na sio kutupiana mapira katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Lazima tuwe wawazi katika suala hili la kutokomeza madawa ya kulevya, tusipofanya hivhyo basi malengo ya kutokomeza litaondoka”alisema.

Akitoa neon la shukurani kwa niaba ya wadau wa Operesheni na Udhibiti wa dawa za kulevya Pemba, Mratib wa Tume ya Kitaifa ya kuratib na udhibiti dawa za kulevya, Omar Juma Mbarouk aliahidi kufanya kazi kwa pamoja na ili kufikia malengo ya serikali.

Alisema mashirikiano ya pamoja kwa wadau hao, yataweza kufikia malengo ya kutokomeza madawa ya kulevya Zanzibar, ikizingatiwa dawa hizo zinaathiri sana vijana.

Akiwasilisha mada katika mutano huo, afisa sheria kutoka tume ya kitaifa ya kuratib na udhibitio dawa za kulevya Daudi Juma Suleiman, aliwataka wadau wenzake kuhakikisha wanazidisha mashirikianao na nguvu zao katika mwaka 2021, ili kufikia malengo ya serikali katika vita vya dawa za kulevya.

AFISA Sheria kutoka Tume ya Kitaifa ya kuratibu na udhibiti wa dawa za kulevya, kutoka Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais, Daudi Juma Suleiman, akiwasilisha mada ya kwanza katika mkutano wa wadau wa Operesheni na udhibiti wa dawa za kulevya uliofanyika mjini Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WADAU wa Operesheni na Udhibiti wa Dawa za Kulevya Kisiwani Pemba, wakiwa katika mkutano wa uwasilishaji wa taarifa za matukio ya Dawa za kulevya kwa mwaka 2020, mkutano uliowashirikisha ZAECA, KM KM, POLISI, DPP na watendaji kutoka Tume ya Kitaifa ya Kuratib na udhibiti wa dawa za kulevya Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
AFISA kutoka Jeshi la Polisi mkoa wa kusini Pemba Issa Abass Mohamed, akiwasilisha taarifa ya dawa za kulevya kwa kipindi cha 2020, wakati wa mkutano wa wadau wa Operesheni na Udhibiti wa dara za Kulevya Pemba, mkutano uliofanyika mjini Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)