Sunday, November 24

Ufahamu ugonjwa wa saratani ya matiti.

 

SARATANI YA MATITI NI NINI?
Saratani ya matiti ni saratani inayowakumba wanawake wengi duniani.
Hatari ya kupata saratani inaongezeka kadiri umri unavyokuwa mkubwa na endapo utaishi miaka 90 hatari ya kupata saratani ya matiti ni asilimia 14.
Mwaka 2007 wanawake milioni 1.7 waligundulika kuwa na saratani ya matiti duniani.
Wanawake 465,000 walikufa kutokana na saratani ya matiti mwaka 2007 duniani.
Marekani ya Kusini, Australia, Ulaya ndiyo mabara yanayoongoza kuwa na idadi kubwa ya matukio ya saratani ya matiti.
Maeneo mengi ya bara la Afrika na Asia yana matukio machache ya saratani ya matiti.
Kuongezeka kwa hatari ya kupata saratani ya matiti kunatokana na: –
• Kuanza kupata mzunguko wa hedhi mapema katika umri mdogo.
• Kupata kipindi cha ukomo hedhi.
• Kurithi.
• Kuwa na unene uliokithiri.
• Matumizi ya pombe.
• Kutokuwa na mtoto.
• Matumizi ya dawa za kuzuia ujauzito.
• Matumizi ya dawa za vichocheo baada ya kufikisha umri wa ukomo hedhi.
• Kurithi vinasaba fulani vya saratani ya matiti viitwavyo (BRCA1 au BRCA2)
Mwanamke atakuwa amepunguza hatari ya kupata saratani ya matiti kwa kufanya yafuatayo :-
• Endapo atanyonyesha vizuri,
• Endapo atakuwa anafanya mazoezi ya viungo,
• Endapo atapunguza uzito,
• Endapo hatotumia sigara au tumbaku,
Saratani ya matiti inaweza kuzuilika kwa kufanya vipimo vya uchunguzi mara kwa mara.
Kufanya mazoezi kwa saa moja kila siku kunapunguza hatari ya kupata saratani ya matiti kwa asilimia 25.
Kupata matibabu ya saratani ya matiti mapema kunaongeza uwezekano wa kuishi miaka 5 kwa asilimia 98.
Wanawake wenye vinasaba vya saratani ya matiti viitwavyo BRCA ambao kokwa zao za uzazi zitaondolewa kwa upasuaji wanapunguza uwezekano wa kupata saratani ya matiti kwa zaidi ya asilimia 50.