NA ABDI SULEIMAN.
VIONGOZI mbali mbali wa vyama vya siasa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi wa Kisiwa cha Pemba, wamesema kuwa suala la kumpata mtu atakae weza kurithi na kufuata nyao za marehemu Maalim Seif Sharif Hamadi litachukua muda mrefu.
Walisema kuwa kuondoka kwakeni ni pigo kubwa Zanzibar, kwani aliweza kuondosha fitna, uaduwi, uhasama kwa wananchi wa Unguja na Pemba,hali iliyopelekea amani na utulivu kutawala katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tafauti, wakati wa mazishi ya aliyekua makamu wakwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi, kijijini kwao Mtambwe Nyali Wilaya ya Wete.
Katibu Mkuu wa Chama cha CUF Tanzania Mussa Haji Kombo, alisema kuondoka kwake maalimu Seif Sharif Hamad ni pigo kubwa Zanzibar, kwani chama sio kinachosababisha mtu kuchukia watu lazima wananchi au wanachama kuondoa chuki na fitna ili kumuenzi kwa vitendo maalim.
“Maalim seif alipokua katibu mkuu wetu wa CUF, hakukua na fitna na alikua mzuri na akizungumza na watu wote, matukio yaliypotokea sio sababu ya uhasama wala uwadunia”alisema.
Aidha aliwataka vijana kusoma mambo mbali mbali aliyokua akifanya maalumu kwa vitendo, kwani mwaka 2010 alikuwa makamu wa kwanza nan chi ilikua katika hali ya amani na utulivu.
Hata hivyo aliwataka vijana kujitahidi kuweka nidhamu mbele katika maisha yao, pamoja na kusoma kwa bidii kwani nchi haiwezi kuwa na kiongozi asiyekua na nidhamu.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Masoud, alisema maalim Seif alikuwa ni kiongozi mzalendo na mwenye mtazamo wa kuwaunganisha wazanzibari na kuwa na serikali ya Umoja wakitaifa.
“Nimtu ambaye siku zote alikua akipigania umoja wa wazanzibari, akiamini kuwa umoja wao ndio utakaoleta mafanikio na maendeleo kwa Zanzibar”alisema.
Hata hivyo aliwataka wananchi kuendeleza kuhubiri suala la amani, hivyo aliwataka viongozi wa chama hicho kuhakikisha wanafuata nyayo zake na hakuna sababu ya kugawana, kutafarukiana badala yake kushirikiana na viongozi waliopo katika kuijenga Zanzibar mpya ya uchumi wa buluu.
Naye Mjumbe wa baraza kuu la chama cha ACT-Wazalendo Taifa Hamad Massoud Hamada, alisema katika maisha yake hawezi kumfananisha na kiongozi yoyote katika kupigania haki, uhuru na heshama za wazanzibari na manufaa na maendeleo ya wazanzibari, kuondoka kwake ni pigo kwa wazanzibari wote.
Hata hivyo aliwataka wazanzibari kuendelea kuvumiliana, kuwa wamoja na kudumisha amani iliyopo nchi, ikizingatiwa kuwa wazanzibari wote ni wamoja.
Kwa upande wake naibu katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Ahmed Nassor Mazurui, alisema katika siku 100 ya serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar, aliyekua Makamu wa Kwanza wa Rais Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad, ameweza kuwaachia hazina kubwa ya umoja, upendo na mshikamano, hivyo wananchi wanapaswa kuutunza na kuweka mbele uzalendo wanchi.