Monday, November 25

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AEKA SAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KUFUATIA KIFO CHA ALIEKUWA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS MAALIM SEIF SHARIFU HAMAD

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amefika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa AbdulWakil Kikwajuni kwa ajili ya kusaini kitabu cha Maombolezi kufufutia msiba wa aliekuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharifu Hamad.
Makamu wa Pili wa Raisi amesaini kitabu hicho  kutokana na kifo cha Maalim seif  kilichotokea siku ya Jumatano ya tarehe 17/02/2021 majira ya saa Tano dakika ishirini na sita (5:26) katika hopital ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salam baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Aidha, Maalim Seif amewahi kuwa Mjumbe wa kamati kuu na Mkuu wa idara ya uchumi na Fedha kupitia Chama cha Mapinduzi katika makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad atakumbukwa kwa moyo wake wa kujitolea katika kuhubiri na kuimaisha umoja wa kitaifa na kuhubiri Amani visiwani Zanzibar na Tanzania kwa Ujumla.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Peponi Amiin.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Febuari 23, 2021.