WAANDISHI wa Habari kisiwani Pemba, wametakiwa kutumia nafasi zao kwa kuandika habari, zinazolenga kuhamasisha vyama vya siasa na wadau mbalimbali, kuwa na mpango wa kutoa elimu ya uraia mara kwa mara na kuacha kusubiri kipindi cha uchaguzi.
Wito huo ulitolewa na mwezeshaji wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wandishi wa habari kisiwani hapa, kufanya uchambuzi wa habari zinazohusu wanawake, demokrasia na uongozi, Sabahi Mussa Said, yalioandaliwa na Chama cha Waandshi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar(TAMWA ZNZ), ZAFELA na PEGAO kwa kushirikiana na Ubalozi wa Norway Nchini.
Alisema ukosefu wa uwiano sawa wa ushiriki kwa wanawake katika nafasi za uongozi, unasababisha matatizo yanayowakabili wanawake kushindwa kupata kwa kuwasemea.
Sabahi alisema kwa muda mrefu taasisi mbalimbali hasa vyama vya siasa, vimekuwa vikikosa utaratibu wa kutoa elimu ya urai kwa wananchi hawa wanawake kwa wakati, jambo ambalo hupelekea wengi wao kushindwa kupata elimu ya kushiriki kupata haki zao za msingi.
“Mara nyingi elimu ya uraia hutolewa pale tu tunapokaribia kipindi cha uchaguzi, jambo ambalo kwa kweli huwakosesha sana wanawake kuelewa haki zao za msingi, hasa kushiriki kwenye uongozi”alisema.
“Ni wakati wenu waandishi kulisemea hili, ili wadau wote wanaohusika ili waweke utaratibu wa kutoa elimu hii mara kwa mara hasa kwa wanawake,” alisema.
Aidha alisema kutokana na dhana potofu iliyojengeka ndani ya
jamii, juu ya mwanamke anayeonekana kuwa jasiri ni wajibu kwa vyombo vya habari, kujikita katika utoaji wa elimu inayolenga kubadili fikra hizo.
Alifahamisha kuwa waandishi wa habari wanajukumu la kuelimisha jamii, ili iweze kubadili fikra za kuamini kwamba mwanamke mwenye ujasiri wa kusimama na kuzungumza mbele za watu hana heshima kwani uthubutu huanza na uthubutu.
Naye mwanaume wakala wa mabadiliko wa kuhamasisha jamii kubadili fikra, juu ya nafasi ya wanawake na uongozi, Moh’d Hassan aliwataka waandishi wa habari kuandaa habari zenye kulenga kupima ubora wa wanawake viongozi ili kuwahamasisha wengine.
Kwa upande wake mwandishi wa habari mwandamizi Kisiwani Pemba Ali Mbarouk Omar, akiwasilisha mada juu ya umuhimu wakutumia data, aliwataka waandishi hao kuhakikisha wanapoandika habari zao, kwani takwimu zinasaidia katika shuhuli za maendeleo n kusaidi wananchi kufahamu zaidi taarifa ya mwandishi husika.
Alisema bado waandishi wa habari wanawajibu wa kuelimisha jamii juu ya suala zima la usawa wa kijinsi, kwa kutumia fursa ya zinazotoka katika vyama vya siasa.
Nao washiriki wa mafunzo hayo, walisema vyombo vya habari vinapaswa kuwa na ajenda maalumu kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii juu ya kuhamasisha wananchake kugombania nafazi za uongozi.
Time Khamis Mwinyi kutoka Radio Jamii Micheweni, alisema kuwepo kwa ajenda maalum katika vyombo vya habari kuhusu elimu ya wanawake na uongozi, itasaidia kuongeza hamasa zaidi kwa
wanawake kujitokeza kushiriki katika nafasi hizo.
“Sisi vyombo vya habari nadhani kwa hili tunahitaji mpango maalum wa kuweka ajenda ya kuwazungumzia wanawake katika uongozi naamini jamii ikisikia taarifa hizo kila siku itawabadili mitazamo yao na hatimaye adhima yetu ya kuwafanya wanawake kuwa viongozi itafanikiwa,”alisema.
Alisema bado mifumo dume kwa jamii ipo, hasa katika vyama vya siasa haitowi usawa wa kijinsia baina ya wanawake na wanaume, kushika nafasi za juu katika vyama vyao.
Lailat Aliy Msabaha kutoka Histi Fm Raido, aliwataka wanaume kuendlea kuwahamasisha wanawake, katika kushika nafasi za uonmgozi, ili wakati wa upachaguzi utakapofika itakuw ani rahisi kwao.