Monday, November 25

Wana Maskani ya Kinazini Mtambwe washauriwa kuitumia maskani hiyo kwa kuandaa miradi ya maendeleo ambayo itawakomboa kiuchumi.

MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Kaskazini Pemba Asya Sharif Omar, akiwashajihisha akinamama wa kinazini Mtambwe, kujikita katika uchumi wa buluu na Vikundi cha ushirika ili kuondokana na umasikini.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).

NA ABDI SULEIMAN.

MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Kaskazini Pemba Asya Sharif Omar, amewataka wanachama wa chama cha Mapindiuzi CCM wa Maskani ya Kinazini Mtambwe shehia ya Mtambwe Kusini Wilaya ya Wete, kuitumia maskani hiyo kwa kuandaa miradi ya maendeleo ambayo itawakomboa kiuchumi.

Alisema serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar, zimeshatoa fursa za kiuchumi kwa wananchi kujiekeza katikla sekta binafsi, katika uzalishaji wa bidhaa mbali mbali zitakazouzika katika masoko ya kibiashara.

Mbunge huyo ametoa wito huo, wakati alipokua akizungumza na wanaCCM wa maskani ya Kinazini Mtambwe, mara baada ya kukabidhi bati 20 na fedha za kununulia misumari kwa uongozi wa maskani hiyo.

Alisema kwa upande wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari imeshatengeneza mazingira mazuri, kwa ajili ya uchumi wa buluu hivyo wananchi wa kinazini, wanapaswa kutumia eneo hilo kwa vile wamezungukwa na bahari kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya baharini.

“Nachukua fursa hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Magufuli na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyi, kwa kuimarisha huduma mbali mbali za kijamii na maendeleo”alisema.

Aidha aliwasisitiza wanachama hao kuitumia maskani hiyo kwa kuimarisha shuhuli za chama, na kuwashajihisha wananchi wengine kujiunga nao ili kuongeza idadi ya wanachama.

“Mtambwe imezungukwa na bahari vizuri kuitumia bahari kupitia mwani, uvuvi, Majongoo na mazao mengine ya baharini ambayo yametuzunguka”alisema.

Kwa upande wake mwanachama wa wakitoa neno la shukurani chini ya mwenyekiti wao Said Hamad Said, wanaCCM hao wamesema kumalizika kwa jengo hilo, wataweza kutumia kwa kubuni miradi inayotekeleza ili kuondosha tataizo la ajira kwa vijana.

“itakapokamilika hii maskani yetu tutaweza kuitumia sisi vijana kwa shuhuli zetu, pamoja na kufanya vikao vya kubuni miradi hapa kwetu tumezungukwa na bahari tutajuwa utuelekee katika mradi upi”alisema.

Naye Mwenyekiti wa maskani ya Hapa Kazi Kinazini Mtambwe Juma Jamaali Fadhili, alimshukuru mbunge huyo kwa msaada alioutoa kwa ajili ya vijana hao, kwani msaada waliopatiwa watautumia ipasavyo.