NA FATMA HAMAD
Wandishi wa habari wametakiwa kutoa elimu kwa vyama vya siasa waweze kutoa fursa sawa za uongozi kwa Wanawake na Wanaume ili kuona Wanawake nawao wanashika nafasi za uongozi katika ngazi mbali mbali za maamuzi.
Hayo yamesemwa na mwezeshaji wa mafunzo ya uhamasishaji wa Wanawake katika ushiriki wa Demokrasia na uongozi kwa wandishi wa habari huko Ofisi za Tamwa mkanjuni Chake chake Pemba.
Amesema imeonekana bado hakuna uwiano sawa baina ya wanaume na Wanawake katika ngazi mbali mbali za maamuzi, hivyo ni jukumu la wandishi wa habari kuwaeilimisha viongozi wa vyama vya siasa kuondosha vikwazo ambavyo vinawakosesha fursa ya uongozi wanawake wenye nia ya kugombea.
‘’Ni jukumu lenu Wanahabari kuwapa elimu viongozi wa kisiasa kuondosha vikwazo vinavyowafanya wanawake washindwe kuwa viongozi’’. Alisema Bi sabah.
Amesema mwanamke ananafasi kubwa ya kuwasilisha matatizo ya jamii yakiwemo ya Wanawake katika vyombo vya mamuzi kwa kulinganisha na Wanaume.
Hivyo ameisihi jamii kuondosha dhana potofu na badalayake waone kwamba mwanamke nayeye anaweza kuwa kiongozi.
Hadia Faki Juma mshiriki wa mafunzo hayo amesema mfumo dume uliopo kwa vyama vya siasa pamoja na jamii umekuwa ukiwakatisha tamaa wanawake walio na nia ya kugombea.
Nae Suleiman Rashid Omar ambae pia ni mshiriki wa mafunzo hayo amesema ni vyema Wanawake kulipa kipaombele suala la Elimumu jambo ambalo litawajengea uwezo wanawake wakati watakapopata fursa za uongozi.
Mafunzo hayo ya siku nane kwa wandishi wa habari yameandaliwa na chama cha wandishi wa habari wanawake Zanzibar Tamwa,