
Na Talib Ussi
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman Sharif amewataka Wazanzibari kumuunga mkono Rais wa Zanzibar katika juhudi za kuleta maendeleo ili ziweze kufanikiwa kwa urahisi.
Kauli hiyo ameitoa leo huko Msikiti wa Muembe Tanga Mjini Unguja wakati alipohudhuria khitma ya kumuombea dua aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad aliyefariki tarehe katika ya mwezi uliopita mwaka huu.
Alisema katika katika kipindi hichi Zanzibar imepata fursa ya kuwa na kiongozi anaetizama mbele hakuna budi itumiwe fursa hio kufikia malengo yaliokusudiwa.
“Tumuunge mkono Rais na Serikali ili iwe rahisi kutatuliwa shida zetu mbali mbali” alisema Makamu huyo.
Alisema hayo yoote hayatofikiwa kama Wazanzibari hawatakuwa kitu kimoja na kuwaomba waendeleze Umoja wa Kitaifa uliopo.
Aliwaambia Wazanzibari walihudhuria katika dua hiyo kuwa endapo watauvunja umoja huo basi itakuwa wamemdhulumu Maalim Seif ambaye alikuwa muumini mkubwa wa Umoja wa Kitaifa.
“Wazanzibar wenzangu dua nyengine kubwa ya kumuombea kiongozi wetu ni kuendeleza yale aliyotuachia ambayo umoja wa Wazanzibari” alieleza Othmani.
Aliwataka kuendeleza upendo ambao umeleta amani Nchini bila kujali vyama vya siasa, dini na rangi.
Akielezea hatua ya yeye kukubali kuwa Makamu wa Kwanza haikuwa rahisi lakini alifahamisha kuwa akulibali sauti ya wengi kwa sauti ya wengi ni kauli Mungu.
“Kwa sababu niliambiwa kuchukuwa nafasi ambayo alikuwa nayo kiongozi wetu mkubwa ambaye akipenda Umoja wa Wazanzibari na mimi sina budi kuendeleza yale aliyotuachia kwa nia safii kabisaa” alisema Othman.
Pia alisema kutokana na Rais aliyepo ni muumini wa Umoja wa Kizanzibari hatopata shida na kazi ambayo Wazanzibar wamempa.
“Kila mtu ni shahid kwa yale maisha na khulka za Mzee wetu na matendo yake kwa jamii yetu ndani na nje” alisema Othaman.
Alisema mikusanyiko ya dua ni dalili kuwa kiongozi huiyo alikuwa na mapenzi makubwa ya watu na kutamka hakuna kubudi kuenzi na kumkumbuka kila wakati.
“Ni wajibu wetu kusimamia ya kuyaendeleza, Mimi nimepewa moja ya dhamana ya kuyaendeleza yale aliotuachia Maalim Seif nawahikishia kwa uwezo wake Allah sitowaangusha” alisema Mrithi huyo wa Maalim Seif.
Alifahamisha kuwa yeye hajapitia yale machungu aliyoyapata Maalim seif katika siasa lakini alikubali kupokea kijiti hicho sio kuwa wengine hawapo, alisema wapo kina Mzee Duni na katika Brand tena Super Brand na wengineo lakini atapata fursa ya kusoma na kujifunza kwao.
Mapema akimkaribisha Makamu wa Kwanza wa Rais, Makamo Mwenyekiti wa chama ACT – Wazalendo Juma Duni Haji alieeleza kuwa Maalim Seif alikuwa akiwapenda wazanzibar kama alivyokuwa akiwapenda watoto wake, licha ya kupata changamoto nyingi wakati uchaguzi lakini alisema hakuacha mapenzi yake kwa wananchi wake.
Alisema katika kuelekea nani awe mrthi wake katimati ya uongozi ya chama hicho ilibebwa na hekma na busara ili umoja uliopo usijeukatetereka.

