Sunday, March 16

MHE. HEMED AZITAKA MAMLAKA ZENYE DHAMANA YA KUSIMAMIA MIJI KUENDELEA KUFANYA KAZI

 

Mamlaka zinazosimamia miji zimetakiwa kuendeleza kazi ya usimamizi wa suala la usafi wa mji ili kuungana na kauli ya Mhe. Rais katika  kupendezesha haiba ya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla  ametoa kauli hiyo katika uwasilishaji wa maelezo ya mradi wa kusimamia usafi wa mji kupitia wazo lililoandaliwa na Kampuni ya VIGOR na kuwashirikisha washauri elekezi kutoka CRM Land Consultancy Limited.
Katika kuhakikisha miradi inayoanzishwa inafanikiwa Mhe. Hemed amependekeza kuwepo kwa ushirikishwaji wa wataalamu kutoka sekta zote kuanzia mwanzo wa mradi ili kupata mawazo yatakayosaidia kukamilika kwake bila ya kutokea athari za kimazingira.
Nae Mwenyekiti wa Kampuni ya VIGOR Mhe. Slum Taufiq Turky amemuleza Makamu wa Pili wa Rais kuwa sekta binafsi zimeamua kuja na mipango ya kuisaidia nchi kutokana na maelekezo yaliotolewa na Mhe. Rais kwa kuzitaka sekta binafasi kushirikiana na serikali.
Akiwasilisha ramani ya mji utakavyokuwa kwa mkoa wa mjini Magharibi Dk. Aleshiwa Clara ameleza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kufanya mji wa Zanzibar kuwa kitovu cha utalii kwa kujenga madaraja ya kuvutia  yatakayopita baharini na kuunganisha na mji mkongwe mji wa Zanzibar.
Wakiwasilisha mada ya udhibiti wa tanga pamoja na mfumo wa usafiri Injinia Jonas Gerevas Balengayabo na Injinia Allbert BModest Mwauzi wamesema taka zinaweza kudhibiwa kwa kuandaa mfumo maalum wa kuzitumia taka hizo katika uzalishaji wa nishati ya umeme pamoja utengenezaji wa Mbolea.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)