Sunday, November 24

Virusi vya corona: Je tunaweza kupata virusi vya corona kupitia macho?

Maelezo ya picha, Inawezekana kupata SARS-CoV-2 kupitia macho

Daktari wa kwanza duniani kufariki dunia kwasababu ya ugonjwa wa Covid-19 alikuwa daktari bingwa wa macho Li Wenliang: na tangu wakati huo, macho yamekuwa yakihusishwa kwa karibu sana na janga la corona.

Ingawa moja ya njia inayofahamika katika maambukizi ya ugonjowa wa corona ni matatizo katika mfumo wa kupumua, lakini pia unaweza kusambazwa miongoni mwa binadamu kwa mikono na kushika maeneo machafu.

Lakini kisichofahamika ni virusi vinavyopatikana katika machozi ya binadamu pamoja, seli za konea na utando wa kamasi.

Kupata maambukizi ya virusi vya corona kupitia macho na machozi ni jambo linalowezekana kabisa.

Virusi vilivyopata maambukizi ya erosoli yaani umajimaji hukutana na eneo la jicho na baadaye huingia katika mfumo wa upumuaji kupitia njia iliyo kama mfereji.

Dalili za macho kupata maambukizi ya virusi vya corona ni zipi?

SARS-CoV-2 umesababisha athari kubwa kote duniani na madhara yake kwa upana bado hayajafahamika wazi.

Ilustración que muestra coronavirus uniéndose a receptores en células humanas

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Seli za binadamu ambavyo virusi vya corona hutumia kuingia mwilini zipo pia katika macho

Uchunguzi wa awali umeangazia sana maambukizi ya njia ya kupumua. Hata hivyo, ushahidi wa maambukizi ya macho unazidi kuongezeka.

Baadhi husababishwa na virusi vyenyewe huku mengine yakitokana na janga ama kwasababu ya mabadiliko ya kimaisha au kwasababu ya watu wanaokaa sana kwenye vyumba vya kuhudumia wagonjwa mahututi ambako wanaweza kuwa huko kwa wiki tatu hadi sita wakitumia vifaa vya kusaidia kupumua.

Hombre con mascarillas frotándose un ojo

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Ni muhimu kuepuka kugusa au kufuta macho yako

Kwa upande mwingine, kujifungia kwa muda mrefu na ulazima wa kutumia barakoa kumeongeza visa vya macho kuwa makavu na magonjwa mengine ya macho.

Maambukizi ya macho yanayotokana na SARS-CoV-2 hutokea sana na yanajumuisha kikope, jicho kuwa kavu, kuwasha, kutoona vizuri na kutostahamili wanga mkali kama wa kupiga picha.

Dalili hizo zinaweza kujitokeza kama ishara za awali za ugonjwa wa virusi vya corona.

Kipindi cha kuatamia cha virusi ni kuanzia siku 5 hadi 14.

Mujer colocándose una lente de contacto

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Unahitaji kuhakikisha mikono yako ni misafi kabla ya kuosha na kuvaa lenzi za macho

Pia wakati wa maambukizi ya macho, neva zinazosaidia misuli ya jicho zinaweza kushindwa kufanya kazi.

Katika visa kidogo pia huwa kunatokea uvimbe kwenye neva za macho.

Lakini mbali na konea, virusi vya corona pia vimebainika kwenye retina za jamaa za waliofariki dunia kwasababu ya maambukizi ya virusi vya corona.

Taarifa zaidi kuhusu corona:

Kipi kinaweza kufanyika kuzuia corona ya macho?

Baadhi ya majarida yameonesha kwamba macho ni njia inayotumika kupitisha maambukizi hadi mwilini na yana uwezo wa kuwa chanzo cha maambukizi.

Persona lavándose las manos

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Licha ya kwamba tuko tatika janga kwa mwaka sasa, tabia ya maambukizi bado haijafahamika wazi. Kwahiyo kunawa mikono ni muhimu.

Licha ya kuwa katika janga kwa zaidi ya miezi 10 bado tabia ya maambukizi hayo hayajafahamika rasmi. Lakini unahitajika kuchukua tahadhari.

Kwa kuzingatia hili, kuosha mikono mara kwa mara ni lazima pamoja na kuepuka kushika na kufuta macho yako.

Hatua hii ni muhimu zaidi kwa wanaovaa lenzi zinazoambatanishwa na mboni.