Monday, November 25

MASHINDANO ya elimu bila ya malipo Wilaya ya Wete kutimua vumbi mwishoni mwa wiki hii

 

NA SAID ABRAHMAN, PEMBA.

MASHINDANO ya elimu bila ya malipo Wilaya ya Wete, yanatarajiwa kutimua vumbi mwishoni mwa wiki hii kwa michezo mbali mbali.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na kamati ya usimamizi wa mashindano hayo katika Wilaya hiyo, imebainisha kuwa mashindano hayo yataanza na mchezo wa Riadha katika Kiwanja Cha Skuli ya Limbani, mchezo utakaoshirikisha skuli zote za kanda ya mjini.

Kwa Upande wa Kanda ya Kati kutakuwa na michezo ya mpira wa miguu Kati ya Skuli ya msingi Kijumbani na Piki, mchezo utakaofanyika katika Kiwanja Cha Skuli ya Kisiwani ‘A’, huku Shengejuu ikiumana na Kiungoni katika Kiwanja Skuli ya Pembeni na Pandani ikivaana na Mzambarauni Takao katika Kiwanja Cha Skuli ya Mzambarauni Takao.

Kanda ya Pwani, Skuli ya msingi Kokota itatoana jasho na Uvinje msingi katika Kiwanja Cha Kokota majira ya saa 2:00 za asubuhi, Mkote kuvaana na Gando katika Kiwanja Cha Skuli ya Utaani, Ukunjwi na Mabatini katika Kiwanja Utaani, Ukunjwi sekondari na Gando Kiwanja Cha Utaani na Mabatini Sekondari kuvaana na Mkote katika Kiwanja Cha Skuli ya Utaani.

Aidha Kanda ya Kaskazini Skuli ya Mgogoni Sekondari itaweza kupambana na Wenzao wa Kinyasini huku Kinyasini msingi itavaana na Mgogoni.

Hata hivyo Kamati hiyo imezitaka Skuli zote, ambazo zitashiriki michuano hiyo kudumisha nidhamu ndani na nje ya mchezo pamoja na kuzitatia kuwa michezo sio uaduwi.

Adha Kamati hiyo imewataka walimu, kushughulikia wanafunzi wao paamoja na kulipia ada ya waamuzi, ambao wataweza kusimamia mashindano hayo, pamoja na kuhakikisha wanafunzi wa skuli za msingi hawazidi umri wa miaka 14,