Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tamwa-Zanzibar DKt,Mzuri Issa Ally amesema waandishi wa habari ni watu muhimu na wenye mchango mkubwa wa kuwasaidia wanawake wa Zanzibar kufikia malengo yao ikiwemo ya kushika nafasi za uongozi.
Aliyasema hayo katika ofisi za Chama hicho zilizopo Tunguu Wilaya ya kati Unguja wakati wa mafunzo ya waandishi wa habari 40 kutoka vyombo mbali mbali.
Mafunzo hayo ya siku mbili yalilenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutambua umuhimu na mchango wa mwanamke kwenye jamii sambamba na matumizi sahihi ya mitandao mkwa waandishi wa habari.
Alisema wakati wanahabari wanatekeleza majukumu yao ya kila hawana budi kukumbuka na kuweka mbele umuhimu wa wanakawake katika habari zao za kila siku kwa kuwa baadhi ya waandishi wa habari husahau wajibu huo.
‘’Nyinyi ni sauti ya wasio na sauti jifunze mafunzo haya kisha nendeni mkayafanyie kazi kwa kuinua jamii ya wanawake.
Awali akifungua mafunzo hayo mjumbe wa TAMWA Bi Ummy Aley aliwataka wanahabari vijana kujifunza kwa waliowatangulia ili waweze kuwa bora zaidi.
Alisema taaluma ya habari ni muhimu mmno ambayo inachangaia kuleta mabadiliko na uwajibikaji katika taasisi mbali mbali iwapo itafanywa vyema.
Awali Mwandishi wa habari mkongwe Zanzibar kutoka gazeti la habari leo Khatib Sleiman aliishukuru TAMWA kuendelea kuwajengea uwezo waandishi wa habari hususani vijana.
Sambamba na hayo Khatibi alizungumzia kuhusu umuhimu wa waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa usahihi mkubwa ikiwemo kuwafikia vyanzo vyao vya habari popote pale walipo.