NA FATMA HAMAD-PEMBA
Mahakama ya Mkoa iliopo Chake chake imemtupa Rumande mtuhumiwa Ayoub Mohd Hamad mwenye umri wa 18 mkaazi wa Likoni kengeja Wilaya ya Mkoani Pemba anaekabiliwa na shitaka la kuingilia kinyume na maumbile.
Baada ya mtuhumiwa huyo kupanda kizimbani akisubiri kusomewa shitaka lake, Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka [DPP] Juma Ali Juma ameiambia mahakama hiyo kuwa tayari upelelezi umeshakamilika linalobakia ni kufunguliwa kesi, hivyo tunaomba mahakama yako ihairishe shitaka hilo na lipangiwe siku nyengine kwa ajili ya kusikilizwa.
Hakimu wa mahakama hiyo Lusiano makoe nyengo amekubaliana na ombi hilo na kesi hiyo itaendelea tena tarehe 15/3/mwaka huu.
Imedaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo siku ya tarehe 23/2/2021 majira ya 5;30 asubuhi, huko Likoni Kengeja wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba Alimuingilia kinyume na maumbile ambapo kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifu cha 133 [a] cha sheria ya adhabu sheria nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.