NA ABDI SULEIMAN.
IMEELEZWA kuwa uhaba wa madara ya kusomea wanafunzi ni miongoni mwa changamoto kubwa inayoikabili skuli ya Michenzani Msingi, hali inayopeleka wanafunzi kuingia mikondo miwili huku darasa moja likiwa na wanafunzi 107 hadi 114.
hayo yamebainika katika hafla ya kukabidhi vifaa mbali mbali vya ujenzi wa banda moja, lenye vyumba vinne vya kusomea kusomea kwa skuli ya Michenzani Wilaya ya Mkoani, vifaa vilivyotolewa na mbunge wa jimbo la Mkoani.
Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo Salum Ali Khamis, alisema skuli hiyo inawafunzi 1724 na vyumba saba vya kusomea ambapo wanafunzi wanaingia mikondo miwili huku darasa moja likiwa na wanafunzi 107 hadi 114.
Aidha alisema licha ya kupata msaada wa banda moja lenye vyumba vinne, pia bado wanahitaji vyumba sita vyengine vya kusomea, ili kuweza kukidhi mahitaji ya skuli hiyo.
“hii fondesheni iliyopo haifai kwa sababu ilijengwa muda mrefu, hata huu ujenzi wake ulijengwa kwa kuunga uunga ila sasa tunahii iliyopo tunataka kuivunja yote”alisema.
Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Mkoani Amran Mohamed Dadi, alisema maendeleo hayo walikuwa wa wakiyatafuta kwa muda mrefu, huku akiwataka wananchi na walimu kuhakikisha wanavilinda vifaa hivyo, ili ujenzi huo uweze kumalizika kwa wakati.
Kwa upande wake mfadhili waujenzi wa mabanda hayo kwa skuli ya Michenzani na Mkanyageni, Mbunge wa jimbo la Mkoani Profesa Makame Mbarawa Mnaya, alisema ujenzi wote kwa skuli mbili unatarajiwa kugharimu shilingi Milioni 31, ujenzi unaotarajiwa kufanywa ndani ya mwezi mmoja tu.
Alivitaja vitu ambavyo amekabidhi ni pamoja na matufali elfu kumi (100,00) yenye thamani ya shilingi 12, mifuko 200 ya saruji yenye thamani ya shilingi Milioni 3, Nondo milioni za milimita 12 tani mbili, Nondo za milimita 10 nondo 14 na nondo za milimita nane nondo nane zote zikiwa na thamani ya shilingi 4.2.
Gharama nyengine ni fedha za mafundi Milioni 9.5 na mchanga na kokota ni milioni 3.2, huku akisema gharama zikiongezeka na fedha ataweza kuongeza ili ujenzi uweze kumalizika kwa wakati, ambapo awamu ya kwanza ni kuhakikisha mabanda yanamalizika na kubakia kuezekwa tu.
“Banda la michenzani vumba vinne na mkanyageni vyumba vitatu tatu litakuwa na uzio ambao utawazuwia wanafunzi kutoka njee na kuzuru, banda la Michenzani litagharimu Milioni 18 na Mkanyageni litagharimu Milioni 13”alisema.
Alisema madhumuni makubwa ni kukabidhiana vifaa vya ujenzi, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi alizozitoa wakati wa kampeni kwa jimbo hilo, tayari wameshaanza maandalizi ya ujenzi wa skuli ikizingatiwa skuli ya michenzani in changamoto kubwa ya madarasa.
Aidha aliwataka wanafunzi na walimu wa skuli zote za jimbo la Mkoani, kufahamu kuwa wajibu wa viongozi wao wajimbo ni kuongeza wingi wa madarasa, ili kupunguza idadi ya wanafunzi kufikia 60 kwa darasa moja, sambamba na walimu kujitahidi kusomesha kwa bidii na kutoa wataalamu zaidi.
Kwa upande wake Diwani wa wadi ya Chokocho Rajab Ali alisema diwani ndio wasimamizi wakubwa wa kazi za jimbo, aliwataka walimu kuhakikisha kusimamia ujenzi huo.
Katibu wa Itikadi CCM Mkoani Abdalla Mohamed Abdalla, aliwataka walimu wa skuli hizo kuhakikisha wanazidisha mashirikia ili kuona majengo hayo yanasimama.
Alisema kukamilika kwa ujenzi huo utaweza kupunguza msongamano wa wanafunzi, katika skuli hizo na kuwafanya wanafunzi kusoma kwa bidii.