Monday, November 25

Virusi vya corona: Je taifa la Tanzania linakabiliwa na mlipuko uliojificha?

Maelezo ya picha, Kaburi jipya katika maziko ya mji mkuu Dodoma

Licha ya ushahidi kuonyesha kinyume, serikali ya Tanzania imeendelea kupuuzilia mbali athari ya virusi vya corona katika taifa hilo.

Hakuna takwimu rasmi

Hakuna takwimu za karibuni kuhusu vifo vinavyotokea Tanzania, na hakuna taarifa zozote zilizotolewa na serikali kuhusu athari za virusi vya rasmi tangu Mei mwaka jana, ambapo takriban visa 500 vya maambukizi vilikuwa vimeripotiwa na vifo 20 kufikia wakati huo.

Serikali imesisitiza kwamba hakuna haja ya kuwa na wasiwasi, na imekuwa ikiwachukulia hatua wale inaowatuhumu kwa kueneza “taarifa za uzushi”.

Rais Magufuli amekataa kutekeleza mpango wa chanjo na badala yake amekuza utumizi wa dawa za kitamaduni

CHANZO CHA PICHA,AFP

Maelezo ya picha,Rais Magufuli amekataa kutekeleza mpango wa chanjo na badala yake amekuza utumizi wa dawa za kitamaduni

Tulipowasiliana na naibu waziri wa afya Godwin Mollel, alitutumia video za mahojiano aliyokuwa ameyafanya awali na vyombo vingine vya habari ambapo alisema utoaji wa takwimu kuhusu visa na maambukizi kila siku unaweza kusababisha madhara zaidi kwani utaeneza hofu na wasiwasi.

Alisema sio kwamba serikali imekuwa haikusanyi data. Alisema hilo limekuwa likifanyika na mwaka 2020 walipodadisi takwimu walizokuwa nazo waligundua kwamba “watu wengi walibambikiziwa kuwa walikuwa na corona kutokana na wasiwasi uliokuwepo”.

Waziri huo aliongeza kuwa kusudi kuu la kukusanya data ni kwa ajali ya wanasayansi kuzichakata na kutoa suluhu.

Mtu akijifukiza nchini Tanzania

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Utumizi wa tiba za kujifukiza zimepigiwa upatu nchini humo

Madaktari wanasemaje?

Madaktari wamezuiwa kuuzungumzia ugonjwa wa Covid-19 hadharani.

hata hivyo, katika hospitali moja yenye shughuli nyingi Dar es Salaam, daktari mmoja aliambia BBC kwamba wameshuhudia ongezeko kubwa la wagonjwa wenye matatizo ya kupumua na dalili zinazoendana na Covid-19 katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.

“Kumekuwepo pia na ongezeko la wagonjwa wanaohitaji oksijeni,” aliambia BBC.

“Hali ni hivyo kila pahali, kwenye hospitali za umma na hospitali za kibinafsi. Baadhi ya wagonjwa wamekuwa hata wakinunua mitungi ya oksijeni kwenda kutumia nyumbani.

“Hauwezi kuandika popote kwamba mgonjwa anaugua Covid-19 kwa sababu serikali haitambui kwamba kuna corona,” anasema.

“Hivyo, unakuwa kwenye kizungumkuti kama daktari. Hakuna pia mwongozo kuhusu matibabu ya wagonjwa wa aina hiyo.”

Katikati ya mwezi Februari , Muungano wa maafisa wa matibabu nchini Tanzania ulitoa taarifa kuhusu ongezeko la wagonjwa walio na matatizo ya kupumua. Lakini mkuu wake Dkt Shadrack Mwaibabmbe , alisema kwamba matatizo ya kupumua huenda ni dalili za magonjwa mengine kama vile pumu, ugonjwa wa moyo ama homa ya mapafu, na sio corona.

Ibada katika kanisa moja mjini Dar es Salaam

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Rais Magufuli ameshinikiza mamombi kufanywa ili kukabiliana na corona

Baadhi ya viongozi wa makanisa wamezungumza

Charles Kitima, wa kanisa la Tanzania Episcopal Conference, amesema kwamba zaidi ya mapadri 25 wamefariki nchini humo katika kipindi cha miezi miwili , wakionyesha dalili zinazohusishwa na corona.

Hii haijawahi kutoka hapo awali , kawaida katika kipindi cha miezi miwili tunaweza kupoteza mapadri watatu au wanne kutokana na umri mkubwa au magonjwa mengine …. inafikia wakati kwamba tunapaswa kukiri kwamba tuna tatizo , ugonjwa wa corona upo.

Je! Picha za setilaiti zinaonyesha athari?

Tulitazama picha za setlaiti kwa muda katika maeneo ya maziko mjini Dar es Salaam kuona iwapo kuna idadi kubwa ya watu waliozikwa zaidi ya ambavyo ilitarajiwa kwa kawaida.

Tulichunguza maeneo ya maziko mjini ikiwemo eneo linalooneshwa katika picha hii hapa chini huko Kinondoni.

Picha za setilaiti za maziko ya Kinondoni mjini, Dar es Salaam Januari 2021

CHANZO CHA PICHA,PLANET LABS

Maelezo ya picha,Picha za setilaiti za maziko ya Kinondoni mjini, Dar es Salaam Januari 2021

Kutoka juu , tulifanikiwa kuona ushahidi wa wazi kuhusu ongezeko la makaburi. Lakini sio jambo lisilo la kawaida kwa makaburi kuchimbwa juu ya mingine – suala ambalo huwezi kulibaini kutoka juu angani.

Na kuna utamaduni katika familia nyingi kuhusu jinsi wanavyowazika wapendwa wao katika vijiji , badala ya maziko yaliotengewa jamii katika miji.

Je mazishi?

Biashara ya mazishi imekuwa na mahitaji ya juu ya majeneza mjini Dodoma
Maelezo ya picha,Biashara ya mazishi imekuwa na mahitaji ya juu ya majeneza

”Tulizungumza na wale wanaohusika katika biashara ya mazishi. Imekuwa uchungu mwingi kuona watu katika idadi kubwa wakizika majeneza”, alisema mmoja ya wafanyabishara wa mazishi katika mji mkuu wa Dodoma , akiambia BBC.

”Nimekuwa nikifanya kazi kwa muda mrefu” , mmoja ya watengenezaji majeneza hayo alituambia.

Mwengine alisema kwamba hana vifaa na kwamba alikuwa akiagiza kutoka maeneo mengine ya nchi.

Dereva mmoja wa basi katika mojawapo ya vituo vya uchukuzi Dodoma alisema kwamba biashara zake nyingi mwezi Januari na Februari zimekuwa kuwabeba watu kwenda mazishini.

Utafiti unaonesha ongezeko la wagonjwa wa corona

Utafiti uliofanywa mtandaoni na kundi la kupigania haki za binadamu Public by Change in Tanzania , umedai ongezeko la wagonjwa kutoka mwezi Disemba na hali hiyo kuwa ya kutisha kufika mwezi Januari na februari.

Utafiti huo uliambia BBC kwamba watu wengi wanasema kwamba wanawajua walio na corona , kulingana na kile ambacho madaktari wametambua kuwa dalili na kuwaambia.

Mbunge mmoja wa chama tawala Zacharia Isaay , amezungumza kuhusu ongezeko la vifo na mazishi katika eneo bunge la Mbulu mjini, kaskazini mwa Tanzania- bila kutaja corona moja kwa moja. Pia amezungumza kuhusu uhaba wa mitungi ya oksijeni na vipumuzi katika hospitali kuu ya Dodoma , ya Benjamin Mkapa.

Tumewaomba wasambazaji wa Oksijeni kuthibitisha iwapo vifaa vyao vimepungua , lakini hakuna aliyejibu.

Watu bado wanaendelea kutafuta dalili

Utafiti uliofanywa na benki ya Dunia katika mataifa duniani umeonesha jinsi watu wanavyotafuta dalili za maradhi hayo kama vile mtu kushindwa kunusa ama kupoteza ladha huku data iliochapishwa ikionesha ongezeko la maambukizi ya corona na vifo.

”Tulitazama data ya Tanzania na kuona ongezeko la jinsi watu walivyo na hamu ya kutaka kujua dalili hizo mwezi Januari na Februari mwaka huu” .

Kuna data isio rasmi ya wagonjwa walioambukizwa corona ili kuthibitisha hilo.

Lakini kutokana na uwiano na mataifa mengine , inaonesha kwamba mwanzo wa mwaka huu , omgezeko la raia wa nchini Tanzania walikuwa wakitafuta habari kuhusu dalili kuu za corona.

Mbinu hii ina mapungufu yake , mojwapo ikiwa imetengezewa watu wanaozungumza lugha ya Kiingereza , na sio kiswahili ambacho huzungumzwa na idadi kubwa ya watu. nchini Tanzania.

Shirika la Afya Duniani WHO lina wasiwasi kuhusu hali na imeitaka tanzania kuanza kuripoti idadi ya wagonjwa wa bviruis vya corona na kusambaza data yake.


Warning: file_get_contents(): http:// wrapper is disabled in the server configuration by allow_url_fopen=0 in /data/40/5/71/99/5397425/user/6768456/htdocs/portal/wp-content/plugins/xt-visitor-counter/xt-visitor-counter.php on line 48

Warning: file_get_contents(http://api.xtrsyz.org/xt-visitor-counter/default.php?domain=www.pembapress.club&time=1732503764): Failed to open stream: no suitable wrapper could be found in /data/40/5/71/99/5397425/user/6768456/htdocs/portal/wp-content/plugins/xt-visitor-counter/xt-visitor-counter.php on line 48