Wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA-Zanzibar leo wanakutana katika mkutano mkuu wa kawaida wa kila mwaka wenye lengo la kujadili maswala mbali ya chama hicho.
Afisa rasilimali watu TAMWA Tatu Ali Mtumwa amesema mkutano huo ni wa kawaida ambao hufanyika kila mwaka na kuwapa fursa wanachama kujua harakati zinazofanyika.
Alisema kupitia mkutano huo wa siku mbili wanachama watawasilishiwa ripoti mbali mbali za utekelezaji wa majukumu pamoja na matumizi ya mwaka mzima wa 2020.
Hata hivyo alisema kupitia mkutano huo wanachama pia watapa kuwasilishiwa mpango kazi wa kiutendaji kwa mwaka mzima wa 2021 ambapo watapa fursa ya kujadili na kuboresha kwa maslahi ya taasisi nzima.
Pamoja na hayo alieleza kuwa mikutano ya wanachama ndio sehemu muhimu ya kujenga taaisi imara ambayo hufanya kazi zake kwa kushirikisha maoni ya watu wengi.
Awali kabla ya kuwasilishwa kwa taarifa za kitaasisi wanachama walipatiwa elimu kuhusu maswala ya afya uzazi pamoja na magoiwa ya kisukari kutoka kwa madaktari bingwa huku lengo kuu likiwa ni kuwajengea uelewa dhidi ya maradhi hayo.