NA FATMA HAMAD-PEMBA.
Timu ya wanaume kumi mawakala wa mabadiliko Kisiwani Pemba imewataka wanajamii kuondokana na dhana potofu kwamba mwanamke hawezi kushika nafasi ya uongozi katika ngazi mbali mbali.
Akizungumza katika mkutano juu ya uhamasishaji wanajamii katika kuwaunga mkono wanawake kwenye nafasi za uongozi mmoja wa wajumbe wa mawakala hao Aizak Maganzi Nzula moshi k huko Chimba shumba ya vyamboni Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Amesema Dini haijamkataza mwanamke kushiriki katika ungozi, hivyo ni vyema jamii kuondokana na mfumo dume ambao unamkandamiza mwanamke asishiriki katika ngazi za maamuzi.
‘’Nataka niwatoe hofu uongozi hauja kwamisha taratibu za kidini.
Amesema wakati umefika kuondosha dhana potofu na badalayake kuwapa nafasi wanawake ili waweze kwenda kutetea shida na kero za wanawake wenzao.
Kwa upande wake Omar Mjaka Omar ambae pia ni mjumbe wa mawakala hao amewataka wanaume kuwapa kipaombele wanawake ambao wanania ya kugombea jambao ambalo litapelekea wanawake hao kushiriki kwa wingi katika nafasi za uongozi.
‘’Sisi wanaume tuwaunge mkono wanawake kwani wanauwezo mkubwa wa kufanya kazi’’ Alisema Omar Mjaka.
Aidha amewataka Wanajamii kuwapatia fursa ya kielimu mtoto wa kike ili aweze kuja kuwa mkombozi wa maisha yake ya hapo badae.
Nae Mratibu wa chama cha Wandishi wa habari Wanawake Tanzania [Tamwa] Ofisi ya Pemba Fathiya Mussa Said amesema lengo la mkutano huo ni kuwahamasisha wanawake waweze kujitokeze kwa wingi majimboni kugombea nafasi za uongozi.