Kisomo maalum cha kumuombea Dua Mfanyakazi wa Kitengo cha Habari Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Marehemu Khamis Ali Khamis {Machenga}kimefanyika mara baada ya Ibada ya sala ya Laasiri katika Msikiti wa Mtaa ilipo familia yake Mpendae kwa Binti Hamrana Mjini Zanzibar.
Waumini wa Dini, familia, ndugu, marafiki, baadhi ya Wafanyakazi wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar walishiriki Ibada hiyo iliyohudhuriwa pia na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla.
Sheikh Salum Juma Faki Maarufu Mudir akitoa nasaha baada ya kisomo hicho aliwaomba Waumini kuendelea kusimamisha dua kwa kuwaombea ndugu na Jamaa zao waliokwisha tangulia mbele ya haki Dua ambayo inakuwa kama sadaka kwa wahusika hao.
Sheikh Mudir alisema vitabu vya Dini vimeshafafanua wazi kwamba miongoni mwa amali zinazowastahiki kuzipata Watu waliotangulia mbele ya haki ni pamoja na dua zinazopaswa kuzidishwa.
Marehemu Khamis Ali Khamis { Machenga} alifariki Dunia asubuhi ya Tarehe 10 mwezi huu katika eneo la Mtule Wilaya ya Kusini akiwa kazini alipokuwa kwenye msafara wa ziara ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ndani ya Wilaya hiyo.
Alizikwa jioni ya siku hiyo katika makaburi ya Mwanakwerekwe baada ya kuonja mauti kama yatakavyokifika Kiumbe chochote katika ardhi na mbingu hizi akiacha Kizuka mmoja na Watoto Wanne.
Khamis Ali Khamis aliyetangulia mbele ya haki sisi akituacha nyuma yake Mwenyezi Muungu ame safari njema amin.
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar