Monday, November 25

Virusi vya Corona: Familia yangu ilitaka kunioza nikiwa na miaka 14

Maelezo ya picha, Abeba: “Familia yangu ilinilazimisha niolewe”

Ripoti mpya ya Unicef iliyotolewa Jumatatu inaonesha kuwa mamilioni ya wasichana walio na umri mdogo wapo katika hatari ya kulazimishwa kuolewa ulimwenguni kote kutokana na janga la corona.

“Familia yangu iliniambia sipaswi kukataa ombi kama hilo, kwani mvulana ambaye alitaka kunioa alitoka katika familia tajiri,” Abeba mwenye umri wa miaka 14 aliambia BBC.

Miezi michache tu iliyopita, alikuwa chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa mama yake na ndugu zake kukubali mchumba, aolewe na kusaidia kupunguza shida za kifedha za familia yake wakati wa janga la Covid-19.

Abeba anataka kuwa daktari lakini katika mji wake wa Gondar Kusini, nchini Ethiopia, elimu yake ya baadaye haina uhakika.

Rabi, 16, bado anasoma shule ya upili huko Gusau, Nigeria, lakini marafiki zake wanne wa karibu wameolewa wakati wa janga hilo, na mama yake anaamini anapaswa kufuata mfano huo.

“Majirani zetu wawili wataoa wiki hii, Insha’Allah. Sikujua tu zamu yangu itafika haraka hivi ,” Rabi alisema.

1px transparent line

Na uwezo wa ndoa ya wasichana wadogo sio jambo geni .Katika muongo mmoja ujao, wasichana milioni 10 zaidi wamewekwa katika hatari ya kuwa ma bi. harusi wakiwa watoto kwa ajili ya Covid, ripoti mpya ya Unicef inaonesha.Kulingana na makadirio ya Unicef, hata kabla ya janga hilo kutokea ilitabiriwa kuwa watoto milioni 100 wangelazimishwa kuolewa katika miaka 10 ijayo.

Lakini sasa takwimu hiyo ni kubwa zaidi, na makadirio ya ongezeko la asilimia 10.

Kufungwa kwa shule ulimwenguni, mtikisiko wa uchumi na kukatizwa kwa huduma za msaada kwa familia na watoto kumezidisha uwezekano wa wasichana kuwa wake kabla ya kufika umri wa utu uzima ifikapo mwaka 2030, ripoti inasema.

Two Fulani girls at an empty school playground.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

“Takwimu hizi zinatuambia kuwa ulimwengu unakuwa mahali pagumu sana kwa wasichana,” Nankali Maksud, mshauri mwandamizi wa Kuzuia Mazoea mabaya huko Unicef, aliambia BBC.

Abeba alisema kuwa aliweza kutoka kwenye ndoa yake iliyopangwa kwa sababu alifaulu kumshawishi baba yake.

“Mama yangu na kaka zangu, waliendelea kunishinikiza niolewe. Mwishowe walitulia wakati familia yangu ilipopata ushauri na maafisa waliwashawishi wabadilishe mawazo yao.”

Lakini kwa Rabi (sio jina lake halisi), tishio bado lipo. Anaishi katika eneo la kilimo huko Damba, makazi ya Wahausa-Fulani kaskazini mwa Nigeria, ambapo msichana mchanga huolewa mara tu anapokuwa na mchumba thabiti.

Bangladeshi women protesting in the capital Dhaka

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Kikundi cha wanawake huko Bangladesh wamekuwa wakipambana dhidi ya ndoa za utotoni

“Kisa changu kilianza wakati wa zuio la kutotoka nje, wakati wadogo zangu walikuwa wakicheza mchezo wa tahajia, na niliamua kujiunga nao,” kijana huyo wa miaka 16 alisema.

Mama ya Rabi alimkasirikia wakati kijana huyo alipopata ugumu katika mchezo huo.

“Alisema,” Umepoteza muda wa kutosha kwenda shule! Angalia ndugu zako wadogo lazima wakufundishe! “

Mama yake aliendelea: “Kufikia sasa, wasichana wote katika mwaka wako wa shule wameolewa. Nitamuuliza Shafi’u [anayemposa Rabi] awapeleke wazazi wake waombe mkono wako rasmi katika ndoa.”

Marafiki zake Habiba, Mansura, Asmau na Raliya waliolewa mwaka uliopita ili kupunguza shida za kiuchumi katika familia zao.

Mwanamke katika eneo hilo ambaye ni rafiki ya mama yake Rabi hakuelewa kusita kwa msichana huyo.

“Mzazi anangojea nini kingine?” aliiambia BBC. “Sina uwezo wa kulipia masomo ya binti yangu. Ndoa ni fursa kwa msichana kuanza maisha yake, na kupunguza watu nyumbani.”

1px transparent line

Mtindo unaoweza kubatilishwa Tangu 2011, idadi ya wasichana walioolewa kabla ya kuwa watu wazima kisheria imepungua kwa asilimia 15 kwa jumla, lakini sasa hatua hiyo ipo hatarini kutokana na janga hilo, ripoti ya Unicef inasema .

“Tulikuwa tukipiga hatua nzuri ulimwenguni katika kupunguza ndoa za utotoni. Bado haitoshi kufikia lengo letu la kuiondoa, lakini tulikuwa tunaenda katika mwelekeo mzuri ,” Bi Maksud alisema.

“Lakini Covid ametuweka mbali zaidi na mkondo wetu. Maisha ya wasichana walio katika ujana ulimwenguni yamezidi kuwa mabaya”.

Kuna mienendo mizuri inayoonekana katika ripoti hiyo, hata hivyo. Ijapokuwa ndoa za utotoni bado ni kawaida katika sehemu zingine za ulimwengu, tatizo hilo linapungua katika sehemu zenye mikakati ifaayo.Na ongezeko la hivi karibuni la idadi inayokadiriwa kutokana na janga hilo linaweza kubadilishwa, wataalam wanasema.

Je, ndoa za utotoni zinaweza kuzuiwa?

A school playground in Africa - a billboard reads "Girls need to study, don't marry them off"

CHANZO CHA PICHA,UNICEF

Maelezo ya picha,shule ndio eneo salama

Wataalam wanaamini ndoa za utotoni zinaweza kuzuiwa kwa hatua za kijamii kwa wakati unaofaa.

“Na mfano bora ni India. Katika miaka 30 iliyopita, India imekuwa na programu kubwa za kitaifa za uhamishaji fedha,” Bi Maksud alisema.

Matokeo yake, familia za Wahindi zimepokea fidia ya kifedha kwa kutowaoza binti zao walio chini ya umri.

Pia, ikiwa ndoa haiwezi kuzuiwa lakini badala yake imecheleweshwa, athari bado ina manufaa kwa jamii.”Hilo ni muhimu sana, kwa sababu tunawaruhusu wasichana hawa kumaliza shule, kuwa na chaguo maishani mwake, kujenga ujuzi, na kwasababu hiyo tuna uwezekano mkubwa wa kumaliza msururu wa umaskini,” Bi Maksud alisema.

1px transparent line

Baada ya janga la Corona

From left to right: Abeba, Mekdes and Wude, three girls from Ethiopia who have avoided getting married before turning 18.

CHANZO CHA PICHA,UNICEF

Maelezo ya picha,Abeba na Mekdes, wakiwa na rafiki yao -wote wamefanikiwa kusitisha ndoa zao

Kuna mambo matatu muhimu ambayo yanahitaji kushughulikiwa ili kubadilisha tatizo la watoto kuwa ma bi. harusi. Bi Maksud aliambia BBC.

Kwanza kabisa, warudishe wasichana shuleni kwa njia salama kabisa,” Bi Maksud alisema, au wapawe nafasi ya kukuza ujuzi kama vile kujifunza biashara au ufundi.

“Tunahitaji pia kushughulikia athari za kiuchumi za Covid katika familia masikini, kwa hivyo mzigo wa kifedha haupunguzwi kwa kuwauza au kuwaoza wasichana.”

Mshauri wa Unicef pia alisema kuwa ujauzito wa utotoni ni kichochezi kikubwa cha ndoa za utotoni.

“Kwa hivyo ni muhimu huduma za afya ya uzazi kuanza tena ili wasichana waweze kuzipata, na kuwa na habari na msaada wanaohitaji ili kuweza kufanya maamuzi yafaayo.”

‘Ushauri nasaha ni kusaidia’

Nchini Ethiopia, Abeba anatarajia marafiki wake watasalia naye shuleni na wataepuka ndoa zilizopangwa kabla ya kuhitimu.

Mekdes, 14, ana ndoto za kuwa mhandisi.

“Wakati tulikuwa tunakaa nyumbani (wakati wa zuio la kutotoka nje ), nilisikia wazazi wangu wakizungumza kunioza kwa mvulana ambaye hata sikumjua,” aliiambia BBC.”Nilisema kwamba sikutaka kuolewa na nilitaka kusoma, lakini hawakusikiliza.

“Nilisubiri hadi shule yetu ilipofunguliwa na nikamwambia mkurugenzi wa shule,” kijana huyo alisema. “Aliwaarifu viongozi wa eneo hilo, na wakawashauri wazazi wangu dhidi ya hatua hiyo.”

Wazazi wake sasa wameapa kutomuoza hadi atakapofikisha miaka 18.

“Huduma ya ushauri inasaidia sana katika jamii yetu. Sasa kuna hata mfumo wa polisi kuwashitaki wazazi ikiwa watakataa na kusisitiza kuwaoza wasichana wa umri mdogo .”