NA ABDI SULEIMAN.
WAZIRI wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Rahma Kassim Ali, ameagiza kusimashwa kazi watendaji wakuu wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Ole-Kengeja yenye urefu wa Kilomita 35, kutoka na fedha zilizotumika kutokuendana na ujenzi wa barabara hiyo.
Waziri alitoa kauli hiyo katika majumuisho ya ziara yake alioifanya ya barabara ya Ole-Kengeja, na kuona baadhi ya kasoro zilizojitokeza wakati wa ujenzi wa barabara hiyo na kujenga shaka, kwamba ujenzi huo haukuwa wa kiwango kulingana na fedha iliyotumika.
Miongoni mwa kasoro ambazo zimejitokeza katika barabara hiyo ni ujenzi usio ridhishwa wa makalavati, barabara kupasuka pasuka, kukosekana alama za barabarani, kukosekana kwa mitaro ya kupitishia maji katika barabara pamoja na mkataba wa ujenzi kuwa na mashaka.
Walioagizwa kusimamishwa kazi katika mradi wa barabara hiyo, ni Msimamizi mkuu kwa upande wa Pemba Injinia Amini Khalid na Mratib wa barabara hiyo aliyepo afisi kuu Unguja Injiania Amina Mohamed Habibu.
Aidha Waziri alisema fedha zilizotumika ni za wananchi na hazilingani na thamani ya ujenzi, hivyo amewaagiza kusimamishwa kazi ili kupisha uchungu.
Waziri huyo alisema watahakikisha miradi yote iliyomo kwenye wizara yao, wanaikagua kwa lengo la kujiridhisha juu ya matumizi ya fedha zilizotumika zinalinga na ujenzi husika, ikibainika kuwa na kasoro hatua zitachukuliwa.
“Hii barabara imejengwa haraka haraka na haina kiwango nimeitembelea lakini sio ujenzi haulingani fedha, lazima fedha za wananchi tuzionee huruma licha ya kuwa mm sio mtaalamu”alisema.
Aidha alisema pia kuna ukiukwaji wa mkataba wa ujenzi na kutilia hofu kwamba haukwenda hata Mwanasheri, huku akitaka mamlaka ya nidhamu kuwasimamisha kazi kwa mujibu wa sheria kupisha uchunguzi na baadha ya kujiridhisha watawaachia, pamoja na hatua nyengine kufuata.
Alisema atahakikisha anaunda tume ya uchunguzi kwa ajili ya kuja tatizo hilo, ikibainika kuwepo kwa watu wengine ambao wameingia katika matatizo hatua kali kufuata.
Kwa upande wake katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Amour Hamil Bakar, alisema kwa sasa wanafanya tathmini ya madai ya fidia zote ambayo yapo wizarani na mengine yapo zaidi ya miaka 20, lakini wameamua kujipa muda ili kuhakikisha wanayamaliza.
Akizungumzia matengenezo, alisema watahakikisha maeno yote ambayo barabara zimekatika watafanyia marekebisho, katika maeneo hayo ili barabara ziweze kuwa katika hali nzuri.
“Maeneo mengi yapo ambao yanahitaki kufanyiwa matengenezo ya haraka kabla ya mvua hazijaja, tutajitahidi kufanya ukarabati na kuwa katika kiwango kizuri”alisema.
Akizungumzia sula la agizo la kuwasimamisha kazi, aliseme watalitekeleza na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria kama agizo la waziri lilivyo.
Naye afisa mdhamini Wizara hiyo Ibarhami Saleh Juma, alisema barabara ya Ole-Kengeja yenye urefu wa KM 35 iliharakishwa sana katika ujenzi wake huku kukiwa na madeni ya wananchi na kuongezeka kwa gharama za ziada ili kukamisha.
Kwa upande wa Injia Khamis Massudi alisema sehemu ambazo zinahitaji kujengwa misingi ya kupitishia maji, watahakikisha wanaijenga kbala ya mvua hazijaanza kunyesha, huku wakikusudia kurudi katika michoro ya ujenzi wa barabara hiyo kuangalia kwa kina baadhi ya vitu, ambavyo hivi sasa vimekua vikijitokeza.
Naye Msimamizi wa ujenzi wa barabara ya Ole-Kengeja, Injinia Amini Khalid, alisema fedha iliyotengwa ya ujenzi wa barabara toka mwanzo ilikua haitoshi na ikijenga kwa kilomita 25, huku akikutana na changamoto nyingi ya ukosefu wavifaa.
Alisema baada ya kupatiwa vifaa 2019 na kazi za ujenzi zikaenda haraka hadi kilomita 25 na kubakia Kilomita 9, baade serikali ikakubali kumailizia na kutenga Bilioni tisa (9) na Bilioni 6 ni ujenzi na bilioni tatu ni kulipa fidia.
“Katika Bilioni sita tulipata bilioni 1.4 na agizo la serikali tumalizie barabara kiwango cha lami, tulifuata na kukamilisha huku tukiwa na madeni mengi”alisema.
Alisema deni la ujenzi shilingi Milioni 541, deni la kokoto ni shilingi kuanzia Ukutini hadi kengeja Kilomita 11 bado hazijalipwa, kwa upande wa fidia walilipa ole, pujini, chambani, Ukutini, kendwa na kengeja yenye thamani ya shilingi Milioni 399, kwa upande wa miti bado haijalipwa hata mmoja ni shilingi Milioni 811, huku gharama zote za ujenzi ni Bilioni 30.
Kwa upande wao wananchi ambao nyumba zao huingia maji katika eneo la Pujini, walisema mvua zinapojengwa maji yote huingia katika nyumba zao na kusababisha kero kwao.
Mohamed Suleiman alisema wameshapeleka taarifa muda mrefu juu ya hali hiyo, lakini bado hakujawa na utekelezaji wowote kutoka kwa wasimamizi wa barabara hiyo.
Ujenzi wa barabara ya Ole-Kengeja hadi sasa umegharibu shilingi Bilioni 30, huku mradi huo ukiendelea kukubwa madeni ya baadhi ya vitu kutokulipwa.