NA FATMA HAMAD-PEMBA.
Kutokuwepo kwa Hakimu wa Mahkama ya Mkoa B’’ iliopo Chake chake Lusiano Makoe Nyengo kumemlazimu Hakimu wa mahakama ya Wilaya Ame Msaraka pinja kughairisha kesi ya kuingilia kinyume na maumbile ambayo inamkabili mtuhumiwa Ayoub Mohd Hamad mwenye umri wa miaka 18 mkaazi wa Kengeja Wilaya ya mkoani Pemba.
Baada ya mtuhumiwa huyo kupanda kizimbani wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka [DPP] Ali Amour Makame amesema shauri hilo lipo kwa ajili ya kusikilizwa na leo tumepokea mashahidi wawili ambao ni Mtoto mwenyewe aliedhalilizshwa pamoja na babake mzazi, ila mheshimiwa hakimu tunaomba kesi hiyo uipangie nsikunyengine kwa sababu Hakimu anayesikiliza kesi hiyo hayupo Mahakamani.
Hakimu huyo wa wilaya ambae amelazimika kughairisha kesi hiyo Ame Msaraka Pinja amesema nakubaliana na hilo na mashahidi mnaonywa mfike mahakamani hapo siku ya 19/ 4/2021 kwa ajili ya kusikilizwa .
Imedaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo siku ya tarehe 23/2/2021 majira ya 5;30 asubuhi, huko Likoni Kengeja wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba Alimuingilia kinyume na maumbile ambapo kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifu cha 133 [a] cha sheria ya adhabu sheria nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.