Monday, November 25

Wanawake wenye mahitaji maalumu waomba fursa sawa katika ngazi za maamuzi.

NA FATMA HAMAD-PEMBA.

Wanawake wenye mahitaji maalum wameitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na Viongozi wa vyama vya siasa kutoa fursa sawa kwa akina mama hao katika ngazi mbali mbali za maamuzi.

Akitoa changamoto ambazo  wanakumbana nazo wakati wanapojingiza katika kinyanganyiro cha kugombaea nafasi za uongozi majimboni, Hidaya ambae ana ulemavu wa viungo  amesema bado wanawake wenye ulemavu wanaekwa nyuma katika nafasi mbali mbali za uongozi.

Bi Hidaya ameyasema hayo katika mkutano malumu kwa Asasi za kiraia juu ya kutoa Ushawishi na Utetezi wa Mwanamke kuwa kiongozi huko Ofisi za Tamwa Mkanjuni Chake Chake Pemba.

Ameeleza kuwa walemavu nawao wana uwezo mkubwa wa kufanya kazi, hivyo wasinyimwe  haki zao kutokana na ulemavu wao.

‘’Kila mtu ni mlemavu mtarajiwa, hivyo basi tupeni nafasi na sisi’’ Alisema Bi Hidaya.

Amesema uongozi ni haki ya kila mtu lakini bado  walemavu  wanawake hawapewi fursa sawa za kimaendeleo jambo ambalo linapelekea kudumaa kwa maisha yao.

Akitoa ushuhuda wakati alipojitupa kwenye kinyanganyiro cha uongozi  nafasi ya Ubunge Viti maalum  kupitia chama cha CCM katika Mkoa wa kusini Pemba waka 2010 ambapo alifanikiwa kupita  chaguzi zote na  alifika mpaka Dodoma kwa mara ya pili kwa ajili ya kuapishwa lakini mwisho wa siku ilipofika usiku  ambapo asubuhi anamkea kwenda kuapishwa  jina lake halikurudi.

Akiwasilisha mada ya Ushawishi na Uhamasishaji ju ya Mwanamke kuwa kiongozi mkufunzi wa mafunzo hayo Ali Mbarouk Omar amesema kila mmoja kwa nafasi yake aunge mkono na kuzipa kipaumbele  jitihada za walemavu  wanawake jambo ambalo litasaidia  kufanikisha ndoto zao.

Kwa upande wake Mratibu wa chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa ofisi ya Pemba Fathiya Mussa Said amesema  ofisi yao imekuwa mstari wa mbele kutoa elimu kwa Tasisi mbali mbali ili kuona wanawake wote wenye nia ya kugombea wamefikia malengo yao.