Na – OMKR
Imeelezwa kuwa uwepo wa vizazi vijavyo unategemea sana ustawi wa Bioanuwai na mazingira kwani dunia imeshuhudia ongezeko la kubwa la Idadi ya watu hali inayopelekea kuongezeka kwa mahitaji ya Bioanuwai za bahari na misitu
Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Bi Daima Mohamed Mkalimoto ameyasema hayo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisiya Makamu wa Kwanza wa Rais Bi Khadija Khamis Rajab wakati akiifungua Warsha ya Mpango wa mahitaji ya usimamizi wa fedha za Bioanuai Zanzibar
Bi Khadija amesema shughuli za kibinaadamu kama vile uvuli uharamu, uharibifu wa matumbawe na ukataji wa miti ovyo umechangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa bioanuwai hatimae kupelekea kutoweka kwa baadhi ya viumbe muhimu kwenye mfumo wa Ikologia
Akitoa salaam kwa niaba ya mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP mtaalamu wa mradi kutoka mpango wa maendeleo wa shirika hilo Ndugu Abbas Kitogo amesema jumla ya Nchi 36 zinashiriki katika mpango huu wenye lengo la kuwa na mfumo mzuri wa ukusanyaji wa fedha
Kitogo amewaambia washiriki wa warsha hio kuwa UNDP katika kutekeleza mpango wa mahitaji ya usimamizi wa fedha za Bioanuai imepanga kufanya shughuli nne ambazo ni kuandaa taarifa na utafiti wa kuangalia sera, taasisi katika suala la uhifadhi wa bioanuai
Aidha kuangalia kiasi gani Serikali imewekeza katika uhifadhi wa Bioanuai, kuangalia mahitaji na mwisho kutengeneza mpango wa kitaifa utakoelekeza wapi waelekee katika kukusanya fedha jambo ambalo ni muhimu katika ulinzi wa Bioanuai
Nae Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Zanzibar Bi Farhat A. Mbarouk amesema lengo la mpango huu ni pamoja na kuangalia changamoto za kifedha katika usimamizi na uhifadhi wa bioanuai na hatimae kuja na mfumo bora utakaosaidia uwekezaji na upelekaji wa bajeti zaidi za usimamizi wa bioanuai na mazingira kwa ujumla
Farhat amefafanua kuwa Ili kuwepo na mafanikio jambo muhimu ni kuweka utaratibu wa kuwashirikisha wadau mbali mbali na ndio maana wamewashirikisha wataalaamu kutoka taasisi tofauti ili kuona maeneo muhimu na kwa kiwango gani kinachotakiwa katika uhifadhi na usimamizi wa bioanui pamoja na kuangalia mahitaji
Viongozi wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kupitia Idara ya Mazingira wameishukuru UNDP Tanzania kwa kuichagua Zanzibar kuingia katika mpango huo wa majaribio wa kutathmini matumizi ya bajeti mbalimbali za program za maendeleo na kisekta katika usimamizi na uhifadhi wa Bioanuai
Mradi wa Mpango wa mahitaji ya usimamizi wa fedha za Bioanuai unaotekelezwa na UNDP na kufadhiliwa na wafadhili mbali mbali ikiwemo Umoja wa Ulaya, Ujerumani, Belgium na Switzaland