NA ABDI SULEIMAN.
KATIBU Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatma Hamad Rajab, amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo tayari kusaidia Vijana, lakini bado tatizo lipo kwa vijana katika kuingia kwenye uchumi wa buluu.
Alisema serikali imewekeza katika uchumi huo, baada ya kuona unafaida kubwa kwa nchi, hivyo ipo tayari kuwapatia mitengo na dhana mbali mbali za kuingia katika uchumi huo.
Katibu Mkuu Fatma aliyaeleza hayo kwa nyakati tafauti Wilaya ya Mkoani na Micheweni, kwenye ziara ya kuangalia changamoto zilizomo katika miradi ya vijana kwenye wilaya hizoo.
Alisema Rais Dkt. Miwnyi anania njema na vijana, lazima vijana tuwe kitu kimoja ili kufikia malengo ambayo vijana wamejiwekea, hivyo aliwataka vijana kujituma ili kuona wanafikia malengo yao.
“Serikali ipo tayari kuoa Elimu, Masoko na mtaji kuwapatia lakini lazima vijana wewe wawe na utayari katika vikundi vyao, tayari tumeshapita katika mahoteli ya kitalii na wametuahidi suala la soko lipo”alisema.
Aidha aliwasihi vijana hao kuacha kutumia kilimo cha aina moja katika shuhuli zao, kwani vipo vikundi vingi ila kinachowarudishia nyuma kulima au kubuni biashara ya aina moja.
Alifahamisha kuwa Pemba kuna vikundi vinazalisha Vitunguu maji, Somu, pamoja na mazao mengine ambayo ni tafauti na mazao mchanganyiko, ambayo yanaingia sokoni na mwisho kushusha soka lake.
Katibu mtendaji baraza la Vijana Zanzibar Khamis Faraji, alisema Serikali imetangaza ajira laki tatu kwa vijana Zanzibar, zikiwemo ajira za uvuvu, ufugaji, kilimo lengo ni kuwashajihisha vijana kuingia katika ajira binafsi.
Alisema vijana watakapoingia katika ajira binafsi ikiwemo hizo za ujasiriamali, wataondokana na mzigo wakubaki mitaania bila ya kujishuhulisha na kazi yoyote na mwisho wake kuingia katika makundi maovu.
Naye afisa mdhamini Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba Salum Ubwa, aliwataka vijana kuwa na utayari wa kujiandaa ili miradi itakapokuja kuweza kunufaika nayo.
Mratiba wa Idara ya Vijana Pemba Ali Mussa Bakari, alisema lengo la Serikali na Wizara kuona vijana wanajiajiri kwa kuinua uchumi wa nchi.
Kwa wao Vijana wamesema kuwa wapo tayari kuingia katika uchumi wa Buluu, iwapo watapatoiwa vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi, pamoja na mafunzo ya ahatu ya mwanzo.
Alisema kwa kiasi kikubwa uchumi huo ndio ambao kwa sasa umeshika kasi, hivyo ni vizuri kwa vijana kupoatia misaada mbali mbali itakayoweza kuwafanya kuelekea huko, pamoja na shuhuli nyengine nyingi.