NA SHEKHA SEIF
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Salama Mbarouk Khatib amewaagiza watendaji wa mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF Kisiwani Pemba kuhakikisha walengwa wanatambuliwa kwa usahihi ili kuondoa uwezekano wa kuwa na walengwa wasiokidhi vigezo.
Muheshimiwa Salama amesema hayo huko katika ukumbi wa Jamhuri Wete katika kikao cha kujenga uelewa kuhusu kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya mpango huo, kilichowashirikisha wadau wa TASAF Mkoa wa kaskazini Pemba.
Amesema mfuko huo umekuja na mpango wa kuzinusuru kaya masikini hivyo ni vyema kwa wasimamizi hao kufuata miko na maelekezo yanayotakiwa ili adhima ya serikali iweze kufikiwa huku akisisitiza kwamba Serikali haitosita kuwachukulia hatua watakao kwenda kinyume na agizo hilo.
Kwa upande wake mtendaji wa Tasaf Makao Makuu ndugu Makaza Manyagula Makaza amesema utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya masikini umewezesha kujikita katika kukuza uchumi wa walengwa.
Naye Mratib wa TASAF Pemba ndugu Mussa Said amesema zoezi la utambuzi wa kaya masikini lina changamoto nyingi hivyo ni vyema kwa watendaji hao kua makini katika kuziainisha na kushirikiana kwa pamoja pale panapohitaji kuzipatia ufumbuzi.
ANGALIA VIDEO HAPA CHINI