Na Judith Mhina-MAELEZO
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Kichezo Mhe. Innocent Bashungwa amewaomba Wahisani kuendelea kusaidia Tasnia ya Habari hapa nchini.
Ameyasema hayo wakati akikabidhi seti 16 za redio zenye thamani ya Euro 172,943.76 sawa na Shilingi za Kitanzania Milioni 400 kwa Shirika lisilo la kiserikali la Mtandao wa redio za kijamii (TADIO) lenye jumla ya redio za kijamii zaidi ya 35 nchi nzima.
“Tunapongeza na kulishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni-UNESCO kwa kuuona umuhimu wa kuhakikisha habari zinawafikia wananchi walio wengi hususan kwa makundi yaliyosahaulika wakiwepo Wanawake na Watoto wa Vijijini, pia tunathamini mchango wenu na tunaomba ushirikiano huu uendelee ili kuhakikisha tasnia ya habari inakua nchi nzima”
akikumbushia mambo muhimu ya kujadiliwa katika mijadala ya siku ya uhuru wa vyiombo vya habari kimataifa, Waziri Bashungwa amesema kuna haja ya kuhakikisha uhuru huo ujikite katika mambo makuu matano ambayo ni uhuru wa vyombo vya habari vinavyofaa, kuendeleza nguvu kazi, mazingira mazuri ya sheria na sdera ikiwa ni pamoja na hali bora kazi, ulinzi na usalama wa waandishi na kujua kufanya kazi za uandishi ikiwa ni pamoja na uelewa wa matumizi ya kidigitali.
Naye Mwakilishi wa UNESCO Nchini Tanzania Bw. Tisso De Santos amesema ili kuhakikisha malengo 16 ya agenda za Mkutano wa Umoja wa Mataifa-UN utakaofanyika Septemba mwaka huu katika makao makuu ya Umoja huo Jijini New York Marekani kwa ajili ya kuamua rasmi kuhusu ajenda ya mwaka 2030 yanafanikiwa Tanzania iwe miongoni mwa nchi zitakazotekeleza malengo hayo ili kufikia lengo la Dunia.
Aidha amesema kuwa lipo jukumu kubwa kwa Tanzania kujadili ajenda hizo za kimataifa ambazo zitakuwa katika kipindi cha mpito katika kuelekea Tanzania yenye mageuzi na maendeleo makubwa ikiwepo Tasnia ya Habari.
Pia Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Bw…..amesema sekta ya habari ni muhimili wan ne hapa nchini Tanzania ikitanguliwa na Serikali, Bunge na Mahakama, huku tasnia hiyo ikifanya kazi ya kutoa taarifa kwenye sekta zote nchini katika kufuatilia mwenendo wa Serikali na utekelezaji wake na maoni ya wananchi kuhusu utekelezaji huo.
Kulingana na kaulimbiu yam waka huu ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari kimataifa ambayo ni Habari kwa manufaa ya Umma, imekuja kwa wakati sahihi ambapo nchi zote duniani zinatakiwa kuwa nchi za kidemokrasia, kuwa na uhuru wa habari kama ilivyo kwa nchi ya Sweden iliyopata uhuru huo mwaka 1776.
“Kwa kuwa Dunia inabadilika kiteknolojia kwa kasi sana kuna umuhimu mkubwa kuwa nan chi zenye demokrasia” amesema.
Aidha amebainisha kuwa nchi ya Sweden ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza tasnia ya habari katika masuala yote yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo na kutolea maamuzi.