NA KHADIJA KOMBO-PEMBA.
Wadau wa kesi za udhalilishaji vikiwemo vyombo vya sheria wametakiwa kuwa na mashirikiano ya kutosha huku wakijitolea kwa moyo wao wote katika kuhikisha wanapunguza au kuondoa kabisa wimbi la kesi hizo nchini.
Wito huo umetolewa na Mratib wa TAMWA Zanzibar Tawi la Pemba Fathi-hiya Mussa Said wakati alipokuwa akizungumza na wana mtandao wa kupinga udhalilishaji Kisiwani Pemba katika mkutano wa kujadili changamato zinazokwamisha kesi hizo ,huko katika ukumbi wa Ofisi za TAMWA Pemba Mkanjuni Chake Chake.
Amesema kutokana na ongezeko la kesi hizo nchini TAMWA Zanzibar imekuwa ikishirikiana na wadau mbali mbali wakiwemo Wanajamii, Jeshi la Polisi ,DPP pamoja na mahakama ili kila mmoja aweze kupata uwelewa wa kutosha juu ya masuala ya udhalilishaji kwa lengo la kujenga nguvu za pamoja katika kulitokomeza kabisa janga hilo.
Kwa upange wake Afisa Programme juu ya kupinga udhalilishaji kutoka TAMWA Zanzibar bibi Zaina Salim Abdalla amesema katika kuzishughulikia kesi za udhalilishaji ni lazima kilammoja kujitolea kwa moyo wake wote huku akiwa tayari kupambana na changamoto mbali mbali zitakazo jitokeza.
Wakielezea juu ya changamoto zinazojitokeza katika kesi za udhalilishaji baadhi ya wajumbe hao wamesema bado kuna Vituo vya polisi havijatoa mashikiano katika mapambano hayo.
Kikao hicho cha kujadili changamoto katika kesi za udhalilishaji kimewashirikisha Mahakimu, Maafisa wa Dawati la jinsia, Wasaidizi wa Sheria wa Wilaya,Pamoja na maafisa wa wanawake na watoto Pemba.
KUANGALIA VIDEO BOFYA HAPO CHINI