Tuesday, November 26

PICHA: Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla Amezinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuri 2021 Mkoa wa Kusini Unguja

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah akizindua Mwenge wa Mbio Maalum za Uhuru 2021 katika Uwanja wa Mwehe Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar Mei 17, 2021.
 MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, akimkabidhi Mwenge wa Uhuru, Kiongozi wa mbio hizo, Luteni Josphene Paul Mwangashi, baada ya kuuzindua rasmi,  jana katika uwanja wa Mwehe Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.
MKUU wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hadid Rashid Hadid, akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kiongozi wa mbio hizo, Luteni Josphene Paul Mwangashi, kwaajili ya kuukimbiza katika Wilaya za mkoa huo.
MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, akisalimiana na Kaimu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, na Michezo, ambae ni Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Laila Mohamed Mussa, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, wakati wa uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, huko Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.
MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, akivishwa sakafu na vijana wa Valantia, Kassim Juma  (mbele) na Khamis Othman Kombo, kabla ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, zilizofanyika katika uwanja wa Mwehe Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.
MKUU wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hadid Rashid Hadid, akitoa salamu za mkoa huo wakati wa uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, zilizofanyika katika uwanja wa Mwehe huko Makunduchi.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chma cha CCM Zanzibar, Abdalla Juma (Mabodi), wakifuraia jambo na Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Act – Wazalendo, Salim Bimani, walipokua wakitambulishwa wakati wa uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, zilizofanyika katika  uwanja wa Mwehe Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, akitoa salamu za Watanzania wakati wa uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, zilizofanyika katika uwanja wa Mwehe Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.
KAIMU Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, na Michezo, ambae ni Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Laila Mohamed Mussa, akitoa maelezo machache kuhusiana na uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, zilizofanyika katika uwanja wa Mwehe Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.
MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, akiwahutubia wananchi wakati wa uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, zilizofanyika katika uwanja wa Mwehe Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.
BAADHI ya Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, walioshiriki katika uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, zilizofanyika katika uwanja wa Mwehe Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.
Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja, wakifuatilia uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, zilizofanyika katika uwanja wa Mwehe Makunduchi.
VIJANA wa Vikosi vya Ulinzi ambao watabeba jukumu la kuutembeza Mwenge wa Uhuru, katika Wilaya 150 za  Tanzania.
(Picha na Abdalla Omar )