Wachezaji watoto wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Brig. Jen Michael Luwongo Mstaafu viongozi na walezi na viongozi mara baada ya kumalizika zoezi la kugawa zawadi kwa waliofanya vizuri katika shindano la (Junior’s golf Tournament) lililofanyika Mei 16,2021 Lugalo.
Mwenyekiti wa klabu Brig Jen Michael Luwongo Mstaafu akimvisha medali Nahodha wa timu ya watoto kwa wasichana Jonada Omuteku mara baada ya kumalizika zoezi la kugawa zawadi kwa waliofanya vizuri katika shindano la (Junior’s golf Tournament) lililofanyika Mei 16,2021 Lugalo.
Katibu wa Mashindano TGU Injinia Enock Magile akimuangalia mchezaji Ibrahim Juma anavyopiga mpira katika viwanja vya gofu Lugalo wakati wa shindano la (Junior’s golf Tournament) lililofanyika Mei 16,2021
Mchezaji Ally Kayombo aliyeibuka mshindi wa jumla wa shindano la (Junior’s golf Tournament) akipiga mpira katika moja ya kiwanja cha gofu Lugalo.
………………………………………………………………….
Mchezaji wa gofu ally kayombo ameibuka mshindi katika mashindano ya golf kwa watoto lugalo junior golf tounament yaliyomalizika jana (16/05/21) katika viwanja vya golf vya lugalo jijini dar es salaam.
kayombo aliibuka na ushindi baada ya kupiga mikwaju ya jumla 66 ikiwa ni baada ya kufungana na mchezaji salehe ramadhani aliyepiga awali mikwaju ya jumla 66 nahivyo kumshinda kwa (countback).
mshindi wa tatu ni rahim ally aliyepiga mikwaju ya jumla 68 huku kwa zawadi kwa waliotoka kundi hilo isack daudi,habiba juma na michael masawe waliibuka washindi.
kwa upande wake mwenyekiti wa lugalo brigedia jenerali mstaafu michael luwongo amewataka vijana hao kuendeleza juhudi iliwawe wachezajibora na tumainiwa wa taifa,
“ uwezo wa kupeleka watoto katika mashindano nje ya nchi tunao kikubwa ni kufikia viwango hivyoni jukumu la walimu ambaoni wachezaji wa kulipwa kusaidiana ili kufikia malengo hayo.
aliwataka wachezaji wa kulipwa kuandaa utaratibu wenye lengo la kila mchezaji wa kulipwa aweze kuchangia klabu kwa kufundisha watoto.
kwa upande wake katibu wa chama cha gofu tanzania injinia boniface nyiti aliipongeza klabu ya golf ya lugalo kwa jitihada zake na kuahidi kuendelea kuisaidia klabu vifaa vya watoto huku wakiahidi pia kumuandalia zawadi mwalimu wa watoto hao wa lugalo athumani chiundu.
naye mlezi wa watoto hao ken mbaya alisema amefurahishwa na mashindano hayo ni matumaini yake wadau nayeye mwenyewe hawatachoka kusaidia kundi hilo muhimu.
kwa niaba ya muasisi wa klabu hiyo mkuu wa majeshi mstaafu jenerali george waitara amesema kinachotekelezwa ni maono aliyoyaona kwa muda mrefu anashukuru yanatimia.
muasisi huyo aliwasikilishwa na dk edmund mdolwa katika hafla hiyo ambayo ilishirikisha watoto 45 na kuendelea kuwataka watumiajia wa uwanja kutambua huo ni uwanja wa watanzania.