Picha na – OMPR – ZNZ.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefarijika kwa mafanikio ya vikao vya Sektarieti ya Kitaifa ya kujadili hoja na Changmoto za Muungano, ambapo jumla ya changamoto nane zinatarajiwa kutatuliwa katika kipindi kifupi kijacho.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, ameyasema hayo wakati alipofanya mazungumzo na Sektarieti ya Kitaifa inayojadili changamoto za Muungano, iliofika Ofisini kwake Vuga Jijini Zanzibar.
Mheshimiwa Hemed, amesema mashirikiano mazuri yaliyopo baina ya Ofisi yake, pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais, ni kutokana na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, aliyowapa watendaji wakuu chini ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunano wa Tanzania, Mheshimiwa Philip Isdor Mpango.
Aidha amemshukuru na kumpongeza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mashirikiano yake , hali ambayo yeye pamoja na ofisi yake imekuwa ni kiungo kikubwa katika kuhakikisha mashirikiano ya pamoja yanapatikana.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, amesema Serikali ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar awamu ya nane, chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dr Hussein Ali Mwinyi, imesisitiza kutatuliwa kwa changamoto hizo kwa maslahi ya wanancji wa Zanzibar na watanzania kwa ujumla.
Mapema Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungno na Mazingira Bi Merry N. Maganga, pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tixon T. Mzonda kwa pamoja wamemuahidi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa Sekretariti hiyo ipo inaendelea na vikao vyake ikiwa ni muendelezo wa kujadili na kuzipatia ufumbuzi hoja na changamoto zilizomo ndani ya Muungano.
Kassim Salum Abdi
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar