Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendeleza ushirikiano waken wa kindugu na Serikali ya Oman katika kufikia shabaha ya kuwaletea maendeleo wananchi wa pande zote mbili.
Mhe. Hemed ameeleza hayo wakati alipokutana kwa mazungumzo na Naibu Balozi mdogo wa Oman Bwana Mohammed Al-Bulushi aliefika Afisini kwake Vuga Zanzibar kwa lengo la kubadilishana nae mawazo juu ya uendelezaji wa wa Miradi ya Maendeleo kupitia Sekta mbali mbali.
Katika mazungumzo yao Mhe. Hemed amesema mbali na athari za Covid 19 ilioikumba dunia ametumia fursa hiyo kuikumbusha Nchi ya Oman kuendelea miradi yote ambayo ilikwama kwa muda ndani ya kipindi hicho cha mpito.
kwa upande wake Naibu Balozi mdogo wa Oman Bwana Mohammed Al-Bulushi amesema Serikali ya Oman inaipongeza serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya nane inayoongozwa na Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kasi ilioanza nayo kwa kuonesha dhamira njema ya kuwatumikia wananchi wake.
Naibu Balozi Mohammed Al-Bulushi amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa serikali ya awamu wa nane imekuwa ikitekeleza mambo yake kwa uwazi na ufanisi mkubwa ikiwa na azma ya kuwasogezea wananchi wa Zanzibar huduma za msingi.
Imetolewa na kitengo cha habari (OMPR)