NA ABDI SULEIMAN.
MBUNGE wa jimbo la Mkoani Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, amsema kuwa ametenga kiasi cha shilingi milioni (17.7/=), kwa ajili ya ujenzi wa banda la vyumba vitano vya kusomea la skuli ya msingi Ng’ombeni B wilaya ya Mkoani.
Hayo aliyaeleza katika hafla ya kukabidhi vifaa mbali mbali vya ujenzi wa banda hilo, kwa uongozi wa skuli hiyo hafla iliyofanyika katika skuli ya Ng,ombeni B mkoani.
Alivitaja vitu ambavyo amevikabidhi ni saruji mifuko 150, matufali 4000, nondo, Mchanga na fedha za Fundi shilingi Milioni 4,000,000/=.
Pro. Mbarawa alisema bado anaendelea na nia ya kutekeleza miradi ya elimu, katika maeneo tofauti ya jimbo hilo ili kuhakikisha watoto wote wanapata nafasi ya kupata huduma ya elimu, kama inavyotaka serikali ya awamu ya nane inayoongwa na Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Profesa alisema utekelezaji wa mradi huo ni matakwa ya Chama cha Mapinduzi, katika shughuli za kimaendeleo kwa wananchi wake hivyo ataendelea kutekeleza kila anapoona nafasi ipo.
“Mwanafunzi anaposoma katika mazingira mazuri, hata ule ufahamu wake unaongezeka na matokeo yake yanakua mazuri na kufikia malengo yake, mimi kama kiongozi wa jimbo nitahakikisha malengo yote yanafikiwa tena kwa asilimia kubwa”alisema.
Alisema skuli hiyo ilikuwa na fondesheni ambayo ya muda mrefu imeshindwa kuendelezwa, hali iliyopelekea kuamua kuikamisha na kujenga banda la kisasa na wanafunzi kusoma.
Aidha mbunge huyo alitawaka wananchi kuachana na itikado zao za kisiasa katika suala la maendeleo, kwani maendeleo hayachagui chama kabila wala dini.
Kwa upande wake mwalimu Mkuu wa skuli ya msingi ngombeni B Amina Juma Mussa, alisema watahakikisha wanachukua juhudi ya kuzisimamia rasilimali zilizoletwa na mbunge huyo, ili kuhakikksha ujenzi huo unakamilika.
Alisema kukamilika kwa ujenzi wa skuli hiyo kutaweza kuondosha msongomano wa wanafunzi madarasani, na kuwafanya walimu kufundisha kwa amani na nutulivu.
Aidha aliwataka wadau wa maendeleo na viongozi wengine, kuendelea kuinga mkono skuli hiyo kwa hali na mali ili kuhakikisha inakia malengo iliyojiwekea.
Kwa upande wake katibu mwenezi jimbo Abdalla mohd Abdalla, alisema ni vyema wazazi na walimu kushirikiana na kuona wanafanikisha, lengo la kuundeleza ujenzi wa mabanda hayo yaliokwama kwa muda mrefu, kwani maendeleo yanapokuja hufaika wote.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi jimbo la Mkoani Hamrani Mohamed Dadi, wameahidi kuusimamia utekelezaji wa mradi huo ili umalizike kwa wakati na wanafunzi wapate nafasi ya kutosha katika skuli hiyo.