Na.Kassim Salum OMPR.
Mwenyekiti mwenza wa Kamati hiyo ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alitoa kwa watanzania muda utakapowadia kushiriki vyema katika zoezi la sense ya watu na makaazi bila ya kujali itikadi zao za kisiasa, kidini, kikanda au tofauti yoyote ya kimaumbile.
Mhe. Hemed alisema kushiriki katika zoezi la sense kwa wananchi ni jambo la msingi kwani takwimu zinalisaidia taifa katika kupanga, kutathmini na kuratibu mipango ya maendeleo ya nchi na kukosa kushiriki katika zoezi hili litawia vigumu kwa taifa kufikia maendeleo jumuishi kwa maslahi mapana kwa watu wake.
Aidha, Makamu wa Pili alieleza kuwa kuengezeka kwa utaalamu wa kuendesha zoezi la sense nchini ni jambo la kujivunia kutokana na sense ya mwaka 2012 kuendeshwa na wataalamu wazalendo ukilinganisha na sense zilizopita katika miaka ya nyuma.
Alifafanua kuwa, mbali na ushiriki wa washirika wa maendeleo katika zoezi la sense nchini lakini ni jambo jengine la kujivunia kuona Serikali ya Tanzania imekuwa ikichangia asilimia kubwa katika kutekeleza zoezi hilo akitolewa mfano mwaka 2002 serikali ilichangia gharama kwa asilimia 70, sense ya mwaka 2012 serikali ilichangia gharama kwa asilimia 90, Na kwa sense ya mwaka 2022 serikali inakadiria kuchangia asilimia 95 ya bajeti yote ya sense.
Alisema uchangiaji huo wa bajeti unaashiria mwenendo mzuri namna serikali zote mbili zinavyothamini na kutambua umuhimu wa takwimu zinazotokana na sense ya watu na makaazi.
Pia Makamu wa Pili wa Rais alisema, Fanikio jengine kubwa Tanzania kwa kushirikiana na wadau imefanikiwa kusomesha vijana wengi katika fani ya TAKWIMU na TEHAMA kwa kufikia kiwango cha Uzamili na Uzamivu jambo linaloashiria zoezi la sense la 2022 litaendeshwa kwa uweledi wa hali ya juu.
“Tuna matarajio makubwa sense ya 2022 itafanyika kwa ubora na weledi wa hali ya juu kabisa kutokana na utalamu uliopo na teknolojia ya kisasa itakayotumika” Alisema Makamu wa Pili.
Pamoja na mambo mengine, Makamu wa Pili alisema serikali ya awamu ya nane kama zilivyo awamu nyengine zilizotangulia inathamini na kutambua umuhimu wa sense ya watu na makaazi katika maendeleo ya watu wake, hivyo viongozi na wananchi wa Zanzibar wako tayari kutekeleza zoezi hilo kwa lengo la kujenga mustkbali wa maendeleo ya Zanzibar na wananchi wake.
“Napenda niwathibitishie kwamba serikali ya mapinduzi Zanzibar inayongozwa na Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi imelipokea zoezi hili la kitaifa na italisimamia na kulitekeleza kwa nguvu zake zote kwa maslahi mapana ya wananchi tunaowaongoza” Alieleza Mhe. Hemed.
Mhe. Hemed alisema kutokana na sense kuwa katika mambo ya Muungano zoezi hilo litaanyika kwa ushirikiano kati ya Ofisi mbili za takwimu akizitaja ile Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali ya mapinduzi Zanzibar.
Wakiwasilisha taarifa za muelekeo wa sense ya mwaka 2022 Mtakwimu mkuu kutokanza Ofisi ya Mtakwimu mkuu Zanzibar Bi Mayasa M. Mwinyi na Mtakwimu Mkuu kutoka serikali ya Jamuhuri ya Muungano Dk. Albina Chuwa walisema sense ya 2022 itakuwa ya aina yake kutokana na mipango na mikakti mizuri iliowekwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ambapo vijana wenye weledi na uzoefu wamekwisha andaliwa.
Kutokana na matumizi hayo ya Teknolojia yatapelekea matokeo ya sense hiyo kutolewa nmdani ya kipindi cha muda mfupi huku ikizingatia vitegezo vya kimataifa.
Aidha, Wakuu hao wa Taaisi hizi wamemuahidi Mhe. Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais kuwa Taasisi zao zimejipanga vyema kwa kuzingatia nguvukazi yay a kutosha walikuwa nayo.
Wakuu hao wa taaisi hizo walieleza kuwa kutokana na serikali ya awamu ya sita ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya awamu ya nane kutambua umuhimu wa sense viongozi wake wameamua kutekeleza zoezi hili kwa vitendo kwa lengo la utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025.
Walieleza kwamba sense ya 2022 itakwenda kuzingatia na kutoa taarifa sahihi zinazohitajika kitakwimu kupitia ngazi ya vijiji,kata, shihia hadi mitaa huku ikizingatia takwimu za watu kielimu, kiafya na kiajira.
“Hakuna serikali yoyote duniani inayopanga mipango yake ya kimaendeleo bila ya kuzingatia Takwimu za watu wake Kielimu, Kiafya na Kiajira” Walieleza wakuu hao wa Taasisi.
Akitoa Salamu kutoka shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia idadi ya watu na Makaazi (UNFPA) Bi Jaqueline MahonAlisema shirika hilo litaendelea kutoa msaada kwa serikali ya Jamuhuri ikiwemo vifaa, ramani pamoja na mahitaji mengine katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kama shirika hilo lilivyoshiriki katika sense zilizotangulia.
Sensa ya watu na makaazi nchini inafanyika kwa mujibu wa kifungu cha 6(2a) cha sheria ya takwimu (Statistics Act) na kwa mujibu wa Katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikiwa sense ni miongozi mwa masuala ya Muungano.