Friday, January 24

HABARI PICHA : MWENGE wa Uhuru kitaifa umewasili kisiwani Pemba.

 

MWENGE wa Uhuru kitaifa ukiwa umewasili katika viwanja vya ndege vya Pemba, ukitokea Mkoa wa Mjini Magharibi na kuukabidhiwa Mkoa wa Kusini Pemba kwa kuanza kukimbizwa kwenye wilaya ya Mkoani.

 

 

MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrassa Kitwana Mustafa, akisoma taarifa ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021 kutoka mkoa huo kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Hafla iliyofanyika uwanja wa Ndege wa Pemba.
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud (mwenyemiwani)akiwaongoza watendaji mbali mbali wa serikali Kisiwani Pemba, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salam Mbarouk Khatib, katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuruki taifa 2021 kutoka Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Masoud (kushoto) akipokea mwenge wa uhuru kitaifa 2021 kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, kwa ajili ya kuukimbiza katika wilaya ya Mkoani na Wilaya ya ChakeChake mkoa wa kusini Pemba.

 

MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Masoud (kulia) akimkabidhi Mwenge wa uhuru Mkuu wa Wilaya ya Mkoani IssaJuma Ali (kushoto) kwa ajili ya kukimbizwa ndani ya wilaya hiyo, ambapo utazindua, kukagua na kuweka jiwe la msingi miradi tisa yenye thamani ya shilingi 240,926,047/=

 

 

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)