Sunday, January 26

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na kufanya mazungumzo na Mfanyabiashara ambaye pia ni Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Mei, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Mei, 2021. Wengine katika picha ni Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo, Waziri wa Uwekezaji Geoffrey Mwambe, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Hamad Masauni, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata pamoja na wajumbe wengine waliombatana na Alhaji Aliko Dangote.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam

PICHA NA IKULU.