Uongozi wa Chama cha Waandishi wa habari Wanawake TAMWA-ZNZ leo umekutana na Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar Mh,Othman Massoud ofisini kwake Migombani mjini Unguja wa ajili ya mazungumzo yaliolenga kujenga mustakbali bora kwa faida ya jamii ya Zanzibar.
Akizungumzia kuhusu mkutano huo Mkurugenzi wa TAMWA Dkt,Mzuri Issa alisema mkutano huo uliokua na lengo la kubadilishana mawazo ikiwemo kuzungumzia ujenzi wa kituo cha jinsia huko Tunguu wilaya ya kati Unguja ambapo kituo hicho kitakapokamilika kitaweza kuwasaidia wananchi wengi Zanzibar ikiwemo kupatiwa elimu ya jinsia, kuzidisha mapambano dhidi ya matendo ya udhalilishaji, kuongeza wanawake kwenye uongozi pamoja na biashara.
Alisema kupitia mazungumzo hayo Makamu huyo wa kwanza alishukuru jitihada za TAMWA ZNZ katika kusaidia matatizo ya kijamii ikiwemo wanawake na watoto na kuahidi kushirikiana na taasisi hiyo katika mambo ambayo Afisi yake inasimamia ikiwemo masuala mtambuka pamoja na utawala bora.
Mh.Makamo pia alisema kituo hicho cha jinsia kitakuwa ni cha uma hivyo ni budi wadau wa maendeleo hasa sekta binafsi kutoa michango yao ya dhati kufanikisha ujenzi huo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Utawala wa TAMWA ZNZ bi Halima Issa Msellem Kituo hicho kimeshajengwa hadi katika hatua ya ngazi ya chini ( ground floor) na kimegharimu jumla ya shilingi milioni 358, 000/= ambapo kilitumia fedha za ndani
TAMWA ZNZ.
Mwenyekiti huyo alisema shilingi milioni 524 zinahitajika ili kukamilisha ujenzi huo katika hatua ya horofa ya kwanza na kumalizia (finishing).
Muhammed Khamis