Wadau wa kupambana na matendo ya udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto Zanzibar leo wanakutana katika ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA zilizopo wilaya ya kati Unguja kwa lengo la kujadili kwa pamoja changamoto zinazosababisha uwepo wa matukio hayo na kitu gani kifanyike.
Mkutano huu wa majadilino unawashirikisha watu kutoka mitandao ya kupinga udhalilishaji,vituo vya mkono kwa mkono,maafisa dawati, jeshi la polisi,mahakimu wa mahakama za mikoa,masheha na baadhi ya wazazi ambao watoto wao waliwahi kufanyia matendo ya udhalilishaji.
Udhalilishaji ni kilio cha kila mtu hatupaswi kubaki kimya lakini kuna haja ya kutonyooshena vidole kila mmoja anapaswa kuwa makini na mtendo haya na ndio maana tupo hapa kwa ajili ya kutafuta njia bora za kutengeneza.“`
Muhamed Khamis
Communication Officer
TAMWA-ZNZ