RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Timu ya Madaktari Bingwa kutoka China ukiongozwa na Dr.Wang Yi Ming (kulia kwa Rais) alipowasili katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na Madaktari hao
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Kiongozi wa Timu ya Madaktari Bingwa kutoka China Dr.Wang Yi Ming, (kulia kwa Rais) akiwa na Madaktari hao walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Timu ya Madaktari Bingwa kutoka Nchini China wanaotowa huduma za Matibabu katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, walipofika Ikulu kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi alikutana na Timu ya Madaktari kutoka China waliopo Zanzibar wakiongoza na Wang Yiming ambapo aliwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa huduma kwa jamii kwa miaka mingi.
Rais Dk. Mwinyi aliieleza timu hiyo ya Madaktari kwamba wananachi wa Zanzibar wanafurahishwa na huduma zao wanaozitoa kwa jamii huku akieleza juhudi wanazozichukua za kutoa mafunzo kwa madaktari wazalendo kwamba hatua hiyo imekuwa ikileta tija kubwa kwa Taifa.
Nao ujumbe huo kupitia kiongozi wao Wang Yiming alieleza kuwa timu hiyo ya 30 ya Madaktari kutoka nchini china jumla yao ni 21 wakiwemo madaktari 18 ambao wanatoa huduma katika hospitali ya Mnazi Mmoja na Hospitali ya Abdalla Mzee.
Wang Ying alieleza kwamba mbali ya kutoka huduma katika Hospitali hizo kubwa hapa Zanzibar pia, wamekwua wakitoa huduma za afya katika jamii zikiwemo hospitali ndogo ndogo ikiwemo kutoa dawa, tiba hasa katika siku za mwisho wa wiki pamoja na kutoa mafunzo ya udaktari kwa madaktari wazalendo.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar