NA KHADIJA KOMBO-PEMBA.
Watu wenye ulemavu wa ngozi Kisiwani Pemba wamewaomba wadau wanaowaunga mkono katika kutatua matatizo yanayowakabili, kuangalia uwezekano wakuwasaidia huduma za uchunguzi wa afya kwani kutoka nana hali zao ni rahisi kupata maambukizo ya maradhi mbali mbali.
Wakizungumza baada ya kupata chakula cha pamoja kati ya watu wenye ulemavu wa ngozi na wanajumuiya ya kimataifa ya maendeleo Zanzibar ZIDO huko katika Skuli ya sekondari ya madungu Chake chake wamesema kutokana na ugumu wa hali zao wanahitaji kusaidiwa uchunguzi wa afya zao pamoja na nyenzo nyengine za kuwakwa mua kimaisha.
Kwa upande wake Mkuu wa Jumuiya hio kwa upande wa Zanzibar ndugu Makame Ramadhan amesema ZIDO iko mstari wa mbele katika kusaidia wananchi mbali mbali lakini wao wenyewe wawe tayari kushirikiana na ZIDO pamoja kuibua matatizo yanayowakabili.
Shughuli hio ya chakula cha pamoja imekuja kufuatia ahadi iliyotolewa na Rais wa Jumuiya hio kutoka Canada bibi Rehana Meral kwa wana jumuiya ya watu wenye ulemavu Kisiwani Pemba kutokan na maombi yao kwa jumuiya hio.
Katika Hafla hio pia ZIDO ilitoa msaada wa vitu mbali mbali ikiwezo Mchele ,Sukari Unga, Maharage, Miwani Kofia za kuzuiya jua pamoja sare za Skuli kwa watoto hao.
KUANGALIA VIDEO BOFYA HAPO CHINI